DULLY SYKES" DIAMOND HAENDI KWA WAGAGA ..HII NDIO SIRI YA MAFANIKIO YAKE"

Jina la Diamond Platinumz mtoto wa Tandale mwenye historia ya kuishi maisha ya ukata, sasa hivi ni moja kati ya majina makubwa kimuziki barani Afrika huku akishiriki kwenye project kubwa kama One Campaign iliyoongozwa na D’Banj huku akipewa mashavu na wasanii wakubwa wa Afrika Magharibi.

Dully Sykes ameuambia mtandao wa Times Fm moja kati ya sababu ambazo zinambeba mwimbaji huyo na kumpeleka kwenye level ya juu ya mafanikio kuwa ni kiu kubwa aliyonayo inayomfanya afanye kazi usiku na mchana huku akiwasumbua maproducer bila kusubiri wamuite studio.

“Wasimuone Diamond anafanya vizuri, Diamond anafika mbali wakafikiria Diamond anafanya kazi kwa kumsubiria hadi producer amuite studio, no sio kweli. Diamond anashinda usiku kila siku studio.” Amesema Dully Sykes.

Dully ameeleza kuwa hata yeye pia hukesha studio akifanya kazi na ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri tangu alipoanza muziki bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo huishia kuporomoka na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.

Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa studio ya 4.12 ameongeza kuwa akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi uwapo juu ni moja kati ya sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa muda mrefu.

“Kama wangekuwa wajanja sasa hivi wangekuwa na vitega uchumi…kitu kama studio ni kama jiko. Unakula kwa kutumia studio. Hata kama mtu haji lakini unaweza kutengeneza muziki kwa kutumia akili yako ukasema ‘leo bwana nimeamka saa kumi ya usiku nina idea yangu hebu ngoja niingie studio nidumbukize hii sauti pengine kesho itanifaa. Na kweli unakaa unapata idea nzuri na unatengeneza kitu kizuri.”
Tags

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa duli ila unaemtetea ni mkundu

    ReplyDelete
  2. We duli acha ukuma au mnaendaga wote?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inawezekana mganga wao m1

      Delete
    2. @dully siku chache zilizopita katika pekuapekua yangu mtandaoni nikakutana na kichwa cha habari halima kimwana anamtafutia au anampeleka DIAMOND kwa waganga nikashtuka halafu nika recall years back nikakumbuka halima alivyokuwa best sana na maimatha those days wakishinda wote mwananyamala na kupelekana kwa mganga kule kisiwani mwananyamala hapa ni dhahiri halima ndio hirizi ya diamond believe it or not but tunaomjua halima that the truth angalieni background yake then mwenye neno asogee mwananyamala ulizia wami bar ukifika halima hapo ni mchafu tu all her family.back to dully unakesha saa ngapi studio wakati tunapishana ITALIAN PUB daily late night unatafuta malaya ukimtuma mpambe wako au turushe picha.?let b honest mbona hatuonyeshwi hivyo vitega uchumi vyenyewe?tunaishia kusikia ooh chief kiumbe kampa gari sasa mbona ainiingii akilini unalipwa dollar elfu 50 or 100 then unakubali unapewa gari kesho unapokonywa kwa kuandikwa magazetini.how dare are you superstar?u call urself superstar ha ha ha ha bongo long way to go.kuweni wakweli jamani ndio maana mnaumbuka mwishoni.guys nani anakumbuka ilivyoandikwa mr nice ana ghorofa.nani aliona hilo ghorofa but what happen Is just history.nawakilisha

      Delete
    3. Kula tano mdau

      Delete
  3. mijitu kwa kutukana sijui mnafaid nini nyie wote mnaotukana ndo mamburula na vilaza

    ReplyDelete
  4. Umeonae yani mijitu badala itoe maoni but inaona matuc ndio dili, kama unaona diamond anafaidi na WW c uende kw mganga, mnazani mafanikio ya cku iz kama zamani mpk kw waganga eeh hovyo nowdays akili na bidii yako ndio mafanikio yako, acheni umbulula WA chuk bnafc

    ReplyDelete
  5. Diamond kashajisemea yeye ni mti wa matunda kama hamuelewi vile nyie sema mwisho mlale mtoto yupo kikaz zaidi mtajiju

    ReplyDelete
  6. mtatukana lakin wengne hata walipofika wenzenu hamko,mnakazi ku2kana 2 hamna lolote mkitaka na nyie muende kwa waganga na hayawahusu

    ReplyDelete
  7. Mtu analiowa milioni 50_100 kwa show moja,,,kwanini ananyang'anywa gari na chief kiumbe au kwanini akubali kuzalilishwa,,Swala la kwenda kwa mganga ni lake binasfi kila mtu ana uamuzi wa kuishi maisha anayoyataka kama ka amua awatumikie waganga na kuwaabudu kimpango wake.

    ReplyDelete
  8. Wivu sio dili,alopewa kapewa iwe kwa mganga au kwa nani mungu ndo anagawa riziki,wangapi wanakesha kwa waganga hawafanikiwi.Riziki kila mtu na yake,kama ni wa mia huwezi pata mia mbili usimalize stress kwa kutukana watu sana wajiumiza tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad