HATI ZA MUUNGANO ZALETA UTATA BUNGE LA KATIBA

 Utata umezidi kuibuka katika Bunge Maalumu la Katiba kutokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa Muungano.

Utata huo, umebainika katika Kamati kadhaa siku moja tangu wajumbe wa Bunge hilo waanze kujadili sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wake.

Jana Kamati namba 2 ilimwalika, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo, lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali. Msekwa aliitwa kutokana na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha, alithibitisha kutokea utata huo na kwamba walilazimika kumuita Msekwa ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa.

Nahodha alisema kwa maelezo ya Msekwa, inaonekana hati ya Muungano ipo Umoja wa Mataifa (UN), kwani kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa na kiti chake UN na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hali kadhalika.

Nahodha alisema baada ya UN kuomba uthibitisho wa Muungano, ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.

Kauli hiyo ya Nahodha inapingana na kauli ya Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad ambaye jana alisema hati hiyo ipo Dar es Salaam na ni moja tu, hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.

“Ile hati ya Muungano ipo Dar es Salaam, lakini tunahofia kuileta maana inaweza kupotea kwani ipo moja tu, sasa ambacho tutakifanya inaweza kutolewa nakala na kuthibitishwa na mawakili na ikaja nakala hapa Dodoma iwapo wajumbe wanahitaji,” alisema Hamad.

Nahodha alipoelezwa juu ya majibu ya Katibu wa Bunge kuwa hati hiyo ipo Dar es Salaam, alishikwa na mshangao na kusema wanamuomba Katibu huyo, aiwasilishe kama ipo.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hapa kuna kitu..........

    ReplyDelete
  2. Wabongo viongoziwao wote wajanjawajanja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata vitu vidogo vidogo but sensitive ni ujanja ujanja tu. Kila mtu mjanja mjanja

      Delete
    2. Hata vitu vidogo vidogo but sensitive ni ujanja ujanja tu. Kila mtu mjanja mjanja

      Delete
  3. hati hiyo anayo nyerere kaburini hahahaha hao ndio viongozi wetu,chezea!!

    ReplyDelete
  4. Kwani lazima kuungana kama hawataki tuwaacheni wabaki na nchi Yao kwasababu gani tunawalazimisha wakati Tanganyika tunaweza kujitegemea wenyewe na Kila kitu tunacho..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usiangalie upande mmoja ndugu, huu Muungano upo kwa ajili ya sababu za kiusalama, kwani muda mrefu vile visiwa mataifa ya nje wanavinyemelea, we endelea kulala hivyo hivyo, we hufikirii kwa nini watu wanakataa muungano usife!!

      Delete
    2. Hili li-sengelema

      Delete
    3. ni kweli bora tu kama vipi na muungano ufe maana ishakuwa tabu kunyemelewa acha wanyemelewe kwa uwezo wa Allah tutaishi kwa amani tu mbona tuko mpakani mwa burundi, rwanda, uganda na kenye na milipuko kila siku na tunaishi sembuse znz, kisa cha kutoana roho ni nn

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad