MAPACHA WALIOTENGANISHWA INDIA WAISHI KWA SHIDA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwezi mmoja baada ya pacha waliokuwa wameungana, Ericana na Eliud kurejea nyumbani mkoani Mbeya baada ya kutenganishwa huko India, imebainika kuwa sasa wanaishi maisha magumu.

Pacha hao ambao habari zao ziliuteka umma, walizaliwa jijini Mbeya, Februari 20, mwaka jana wakiwa wameungana kiunoni na kuwafanya washindwe kuonana sura hadi baada ya upasuaji huo.

Pamoja na furaha ya kuonana sura, Gazeti la The Citizen, limeripoti kuwa pacha hao wamekutana na hali ngumu ya maisha kutokana na uwezo mdogo wa familia yao, ikielezwa kuwa wakati mwingine hata mlo unakosekana.

“Maisha ya sasa si kama ilivyokuwa India ambako walikuwa wanakula vyakula vizuri, wanalala pazuri, hapa ni bahati nasibu hata kupata milo mitatu. Muda mfupi ujao hata unga wao wa uji utakwisha, limebaki kopo moja tu,” alisema baba yao mzazi, Erick Mwakyusa ambaye ni dereva wa bodaboda.

Mwakyusa alisema alipopata taarifa kuwa mke wake atajifungua pacha, alipata wakati mgumu kwani alijua hali ngumu waliyonayo, lakini alichanganyikiwa zaidi baada ya kuambiwa kuwa pacha hao wameungana pia.

“Kulea pacha ni jambo moja, lakini kulea walioungana ni ngumu zaidi, sikujua ni jinsi gani nitawalea katika hali waliyokuwa nayo,” alisema Mwakyusa.

Katika changamoto za kutafuta matibabu, Mwakyusa alisema alipotezana na familia yake wakati mkewe Grace alipokwenda Dar es Salaam kutafuta matibabu na baadaye akapata msaada kwenda India alikokaa kwa miezi tisa.

Mwakyusa ambaye ameikodi pikipiki hiyo kwa ajili ya kufanyia biashara anasema hutakiwa kukabidhi kiasi cha Sh6,000 au 8,000 kwa siku.

Kutokana na udogo wa chumba wanacholala, Mwakyusa na Grace hulazimika kulala chini kwenye godoro na kuwaachia watoto wao wawili kitanda cha futi tatu kwa tano. “Licha ya ugumu huo wa maisha, tunaishukuru Serikali kwa kutusaidia kufika India na kututakia mema,” alisema Mwakyusa.

“Tunalala njaa mara kwa mara, ingawa watoto wametibiwa na ni wazima, lakini bado tuna changamoto za kuwafanya wawe hai,” alisema.

Grace alipoulizwa anataka msaada wa aina gani, alisema, “Ningepata Sh150,000 ningefanya biashara,”

Kutokana na kauli hiyo, Balozi wa Kenya nchini, George Owuor alifika katika Ofisi za Mwananchi na kuahidi kutoa fedha alizohitaji Grace kwa ajili ya biashara na wafanyakazi wa ubalozi huo kukusanya fedha kwa ajili ya kununua bodaboda ya baba wa watoto hao ili aachane na kukodi kwa tajiri.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jamani maisha magumu kwa kila mtu madam baba yao ni dereva ajitahid watoto wapate lishe.kila mtu ugumu wa maisha anaoo.au anataka aendelee kuhudumiwa na serikali mbona balaa sasa.

    ReplyDelete
  2. Tuwachangie jamani hali ni ngumu kweli lakini isitufanye tutupane

    ReplyDelete
  3. this is too much,kuzaa mzae wenyewe kulea muombe msaada,si mshasaidiwa operation?? kila mtu ana matatizo aisee!!

    ReplyDelete
  4. hali ngumu kwa kila mtu! kwani hao watoto ni ugonjwa kwake c alipanga kuzaa na Mungu akamjaalia pacha japo walikya na natatizo yaliyonzidi na alisaidiwa watoto wako vzr.nivp tena ulalamike kuhusu majukum yako?hivi wa Tz tukoje? usaidiwe hadi kutunza family yako?ww wajibu wako ni nn? wangapi wabashida? jamani ushikwapo shikamana! ulushikwa mkono kwa tiba ya watoto kuhusu kula,kuvaa na mahitaji yao muhim ni wajibu wako km mzazi!

    ReplyDelete
  5. alafu unasema maisha siyo km india hv unaakili kweli basi ungekaa hukohuko na km mkoa wa mbeya umebarikiwa kwa vyakula namatunda yako mengi unataka nini tena.

    ReplyDelete

Top Post Ad