HII NDIO BONGO, WALIO TIMULIWA MALIASILI WARUDISHWA KAZINI

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

VIGOGO wa Wizara ya Maliasili na Utalii, waliotimuliwa kazi hivi karibuni na Waziri Lazaro Nyalandu, wamerejeshwa kazini.

Taarifa za ndani ya Wizara zilizofikia gazeti hili jana, zilieleza kuwa vigogo hao, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Jafari Kidegesho, walikabidhiwa barua za kurejea kazini jana.

Gazeti hili lilimtafuta Msemaji wa Wizara hiyo, Nurdin Chamuya ambaye hakukanusha wala kukubali kuhusu hatua hiyo, na badala yake alisema alikuwa katika kikao tangu asubuhi hivyo apewe muda amtafute Katibu Mkuu, Maimuna Tarishi.

Baada ya muda, Chamuya aliwasiliana na gazeti hili na kusema kuwa ameshindwa kuwasiliana na Katibu Mkuu, kwa kuwa yuko katika vikao vya Bajeti na hivyo atatoa taarifa kama suala hilo lipo baadaye. Nyalandu alimuondoa Profesa Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Alisema amechukua hatua hiyo kutokana na kutokuridhishwa na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini. “Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa.

“Aidha, ninamuondoa Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dk Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo,” alisema Nyalandu wakati akitangaza hatua hiyo.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa watendaji wote waliokaimishwa nafasi za vigogo hao wamepewa barua na Katibu Mkuu kurejea kwenye nafasi zao za zamani. Gazeti hili lilimtafuta Katibu Mkuu, lakini simu yake iliita bila majibu huku simu ya Nyalandu ikikosekana.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WAWE WANAACHA SIFA ZA KIJINGA KINA NYALANDU WAKATI HAWAYAWEZI ! TUMESHAJUA NCHI HII INAWENYEWE ACHA SISI TUWASINDIKIZE

    ReplyDelete
  2. Ili wazidi kufanya madudu zaidi. Ya uwaji wanyama na mengine mengi. Ya kifisadi. Wanatuharibia. Nchi hawa viongozi vihio. Elimu yao ya uyaga uyaga tu. Kwanza hawajitambui hata kidogo

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni kashfa kubwa kwa mh Nyalandu, kwamba ama alikurupuka ama hakuwa sahihi...AJIUZULU

    ReplyDelete
  4. mh nyalandu presidential appointments haziguswi ki hivyo

    ReplyDelete
  5. Mmmh sipati picha pale wizarani mpingo house kati ya hawa walorudishwa na mh waziri.

    ReplyDelete

Top Post Ad