RIPOTI:IMEBAINIKA KUWA WAWINDAJI HALALI NDIO WANAO UA TEMBO

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Ongezeko la kasi ya ujangili nchini limedaiwa kusababishwa na vitendo vya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na mfumo dhaifu wa usimamizi wa sheria katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Kwa mujibu wa ripoti iliyopewa jina la Urasimishaji wa Ujangili wa Kitaalamu Afrika, tangu mwaka 2000 wizara hiyo imejikuta katika kashfa za rushwa na kusababisha mawaziri na watendaji wakuu kuvuliwa nyadhifa zao.

Katika ripoti hiyo, Taasisi ya Kimarekani ya Utunzaji Wanyamapori ya Born Free USA kwa ushirikiano na Shirika la Ripoti za Kichambuzi na Takwimu la C4ADS, imeeleza pia jinsi vikundi vya waasi barani Afrika wanavyoendesha shughuli za ujangili.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa mwezi huu nchini Kenya, inaitaja Tanzania kama kitovu cha kusafirisha pembe za ndovu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikishindana na ile ya Mombasa katika kutumia bandari kibiashara.

Kutoka mwaka 2008 mpaka 2013, inaelezwa zaidi ya tani 20 za pembe za ndovu ama zilikamatwa zikisafirishwa kuingia au kutolewa katika Jiji la Dar es Salaam, hii ni kwa mujibu wa taarifa ya Taasisi ya C4ADS.

Ripoti hiyo inafafanua kuwa uchunguzi wa vinasaba (DNA), katika tani 11 za pembe za ndovu zilizokamatwa Taiwan, Japan na Hong Kong mwaka 2006, ilibainika kuwa pembe 1,500 zilitoka Tanzania (Selous).

Uchunguzi huo ulibaini kuwa vinasaba vya pembe hizo vilifanana, hivyo kujenga dhana kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiwinda katika hifadhi hiyo mara kwa mara katika utaratibu maalumu unaotambuliwa na Serikali.

“Kuna udhaifu mkubwa katika usimamizi wa uwindaji halali na wawindaji wenye vibali hawasimamiwi ipasavyo kufanya uwindaji kwa taratibu zilizowekwa kisheria. Hivyo hutumia nafasi hiyo kufanya vitendo vya ujangili,” inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Serikali yakanusha

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Paul Sarakikya alikanusha madai hayo akisema siyo kweli kwamba wawindaji halali huachwa bila usimamizi, bali wana mifumo ya kusimamia shughuli hiyo.

“Sikubaliani na ripoti hiyo, tumeshaongea sana juu ya suala hili, Rais alishalizungumzia na waziri pia. Ufafanuzi ndio huo, hamna ukweli wowote katika ripoti hiyo,” alisisitiza Sarakikya.

Salakikya alisema idadi ya tembo nchini inazidi kuongezeka katika hifadhi tofauti na upungufu unaoelezwa katika ripoti hiyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo sarakikya nae anausika kwa asilimia kubwa sana!viongizi wa nchi hii mmezid kutuibia rasilimali zetu cos mnatuona wadanganyika ni maboya tu!kifupi ni kwamba viongozi wakuu wa serikali hii ndio vinara wakubwa na wezi wa pembe za ndovu.Kinana upoooo kuma nyoko.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hahahaha kama wenyewe ndio wezi unategemea nani atalinda?

      Delete

Top Post Ad