Majambazi Wawili Wameuawa Jijini Dar es Dalaam na Wananchi Katika Tukio la Uporaji Eneo la Benki ya NMB Wilaya ya Ilala.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watuhumiwa wawili wa ujambazi wameuawa jijini Dar es Dalaam na wananchi katika jaribio la kufanya tukio la uporaji katika eneo la benki ya NMB Wilaya ya Ilala.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakijaribu kumpora mteja aliyekuwa ndani ya benki hiyo akichukua fedha kwa kutumia silaha mara baada ya kutoka ndani ya benki hiyo.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao ambao idadi yao haijafahamika walifika katika eneo la benki hiyo tawi la Uwanja wa Ndege wakiwa na pikipiki tayari kufanya tukio hilo.
“Hawa walikamatwa kufuatia taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna watu wenye pikipiki ambao wanahisi wanataka kufanya uhalifu. Polisi waliweka mtego nje ya benki lakini waliwashtukia polisi na kuanza kukimbia kila mmoja kwa njia yake,” alisema.
Alisema wakati wahalifu hao wakikimbia, mmoja alifyatua risasi kwa lengo la kupambana na askari, lakini askari hao walifyatua risasi juu kwa lengo la kumuamuru asimame.
“Walifanikiwa kumkamata na alipopekuliwa alikutwa na bastola aina ya Browing yenye namba 230787 iliyotengenezwa nchini Chekoslovakia ikiwa na risasi tatu. Hata hivyo wananchi waliokuwa wengi waliwazidi nguvu polisi wakamshambulia.
“Walimshambulia kwa mawe lakini polisi walifanikiwa kumuokoa na kumkimbiza hospitali lakini alifariki akiwa njiani,” alisema Kova.
Alisema jambazi mwingine ambaye alikimbilia katika eneo la Karakata, wananchi na askari walimkimbiza, lakini hakusimama hata askari walipopiga risasi juu kumtaka asimame.
Alisema baada ya polisi kuona mtuhumiwa huyo anakaidi agizo la kusimama, walimpiga riasasi miguuni na alianguka na kuishiwa nguvu kabla ya kufariki akiwa njiani kupelekwa hospitali.
Kova alisema baadaye jioni jana, watuhumiwa wengine watatu walikamatwa. Aliwataja kuwa ni Salum Seleman (28), Samwel Clips (32) na Said Salehe ambaye ni mganga wa kienyeji.
Alisema Seleman na Clips walikamatwa katika Kituo cha Polisi cha Stakishari baada ya kugundulika kuwa ni watuhumiwa wa ujambazi katika tukio hilo, ambalo wenzao waliuawa.
“Hawa walifika kituoni pale wakiwa wamebadili nguo na kujifanya ni wateja wa kawaida, lakini lengo lao ni kuangalia hatma ya wenzao, lakini waligundulika kuwa nao walishiriki na baada ya kuwakamata na kuwahoji wamekiri kuhusika na wao ndiyo walikimbia,” alisema.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad