Mzee wa Upako Anthony Lusekelo Adai Kuteswa na Misukule

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 MBALI na Askofu wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship, Zacharia Kakobe kuteswa na misukule inayodaiwa kufufuliwa na baadhi ya makanisa ya kiroho nchini, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ (pichani) naye ameibuka na kucharukia suala hilohilo.

Akizungumza na Uwazi juzi, Mzee wa Upako alisema suala la misukule linamtesa sana na kwamba anapingana na kufufuliwa kwao na baadhi ya wachungaji wa makanisa mbalimbali wanaojigamba kufufua misukule wakati si kweli na ni utapeli mtupu.

MZEE WA UPAKO ANAFUNGUKA:
“Kuna baadhi ya viongozi wa makanisa ya kioroho (bila kutaja majina)  wanadanganya  watu kuwa wanatoa misukule, si  ukweli kabisa ni uongo. Wanatafuta  namna ya kula sadaka za waumini wao kwa kuonekana wanaweza sana mambo ya kiroho,” alisema Mzee wa Upako na kuongeza:

“Hawa wachungaji wanatuchafua sana sisi tunaosimamia Neno la Mungu, wanaharibu Kanisa la Mungu kwa kudanganya waumini wao kwa sababu ya pesa tu. Hebu fikiria kuna wengine wanatoa hadi  shilingi 400,000 kwa mtu ili akubali kufanywa msukule feki na baadaye aombewe kanisani tena nimesikia wanatengenezewa hati za kifo kuonesha kuwa kweli watu hao walifariki dunia wakati si kweli, wamwogope Mungu.

“Huo ni usanii ndani ya Kanisa la Mungu. Nasema naumizwa sana na wachungaji wa namna hii, nateseka sana na hili jambo. Ninayo mpaka CD za mahubiri za  baadhi ya viongozi wa makanisa wanaodanganya kuwafufua misukule lakini kwa busara siwezi kuwataja ila wanajijua kwa sababu hata dhamira zao zinawashuhudia.”

TURUDI KWA KAKOBE
Akikazia zaidi, Askofu Kakobe alisema, anayedai ana uwezo wa kufufua misukule ni muongo na kwamba atakuwa anaabudu shetani.

“Mwenye uwezo wa kufufua ni Yesu Kristo pekee na alifanya hivyo kwa sababu ya utukufu wa Mungu na si vinginevyo, si  binadamu wa kawaida ambaye amepewa upako wa Mungu anadanganya watu kuwa anao uwezo wa kumtoa  mtu ambaye alichukuliwa msukule,” alisema Askofu Kakobe huku akisisitiza kwamba mtumishi yeyote wa Mungu anaweza kufanya muujiza huo kwa utukufu wa Mungu lakini si kwa sababu ya kuonesha yeye anaweza.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. uwiiiiiii ni shida ujio wa dajar huo kama mtumishi ni mfufua misukule aende makaburini na mortuary na si Makanisani au kwenye viwanja vya mikutano mbuzi wao km hawana kweli ya mungu wataumbuka soon wala sio la kuficha ni huyo ngwajima mvunja ndoa za watu hana mungu thus why anaboronga hahahaaaaaa flora mbasha utaipata!!!!

    ReplyDelete
  2. Mimi si Kama Wale"

    ReplyDelete

Top Post Ad