Mahakama ya A. Mashariki Yatengua Ubunge wa wabunge wa EAC kutoka Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni muda mfupi uliopita jopo la majaji wa mahakama ya Afrika mashariki huko Arusha imetoa uamuzi wa Shauri ambalo ilifunguliwa na CHADEMA ( Antony Komu ) aliyekuwa mgombea wa Chadema katika Bunge la Afrika mashariki , ambaye alifungua kesi ya msingi kuhusu kukiukwa kwa hati ya makubaliano ya Afrika ya mashariki , kutokana na Chadema kutokupata nafasi wakati hati iko wazi na imeelezea kinagaubaga jinsi ya kupata wawakilishi kutokana na uwiano wa vyama katika mabunge ya nchi washirika .

mahakama ya Afrika mashariki , imesema kuwa Bunge na serikali walikiuka hati hiyo ibara ya 50 , na pia kitendo cha kumpa fursa kugombea John Lifa Chipaka wakati chama chake hakina mbunge ni muendelezo wa kukiukwa kwa hati hiyo ya Afrika mashariki .

Jopo la Mawakili wa Chadema lilikuwa likiongozwa na Edson Mbogoro , Aidha mahakama imeitaka serikali kulipa Antony Komu gharama zote za kesi .

Huu ni muendelezo wa CCM kujidhalilisha kwa kutumia mabavu kwani mliofuatilia mtakumbuka kuwa kulikuwa na ubishani mkubwa sana wa kikanuni ndani ya Bunge siku ya uchaguzi huo, hukumu hii itasaidia sasa ile kesi ya pili ambayo iko mahakama kuu Dodoma ya kuitaka mahakama hiyo itengenezwe uchaguzi ule na irudi we upya kuendelea kwa kasi .
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera sana Anthony Komu kwa kupigania haki yako!!

    ReplyDelete
  2. Watanzania mmeona wenyewe maubauvu ya ccm?? mwenye macho aambiwi tazama!!!

    ReplyDelete
  3. Tena wamezidi pumbavu zenu ..kaziukandamizaje.....hongera jembe

    ReplyDelete

Top Post Ad