Okwi wa Kazi Gani Jaja Mpango Mzima, Mashabiki wa Yanga Wakejeli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TRAIKA mpya Mbrazili aliyekuwa akikejeliwa na mashabiki wa Yanga, Genilson Santos ‘Jaja’ jana Jumapili amepiga bao mbili kati ya tatu zilizoipa ushindi timu yake dhidi ya Azam na kushangilia kwa ishara ambazo mashabiki walizitafsiri kwamba alikuwa akiwauliza; “Okwi wa kazi gani Yanga?”

Awali kabla ya dirisha la usajili halijafungwa kulikuwepo na mzozo baina ya Kocha Marcio Maximo na uongozi wa timu uliotaka straika aliyejiunga na Simba, Emmanuel Okwi abaki Yanga na Jaja akatwe kwa madai kwamba ni mzito na hayuko fiti kama Okwi aliyelipwa fedha nyingi.

Lakini Maximo akashikilia msimamo wake kwamba Jaja ndiye chaguo lake na Okwi hatacheza Yanga kutokana na utovu wa nidhamu na kususa mara kwa mara.Licha ya kuwathibitishia Yanga kwamba yeye ni mashine na amesajiliwa kwa ajili ya kufunga tu, Jaja jana aliwaziba midomo mashabiki wa Simba ambao walikuwa wakimzomea siku za nyuma kwa madai kwamba ni mzito na hana lolote.

Katika mchezo huo wa Ngao ya Hisani uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa huku kipa wa Yanga, Deo Munishi ‘Dida’ akidaka kwa mbwembwe na sarakasi kuwakejeli Azam ambao walimtema, Jaja alipiga mabao mawili katika dakika za 56 na 65. Bao la tatu lilifungwa na Simon Msuva aliyeingia kuchukua nafasi ya Nizar Khalfan katika dakika ya 87.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eeeh,kwa Maximo mchezaji kama hana nidhamu ni kutimua tu,haangalii majina.
    Okwi okwi WA KAZI GANI?Apeleke jeuri yake msimbazi,kwanza ana
    tabia mbaya,namfananisha na mwanamke mwenye kuolewa vyungu 6.

    ReplyDelete
  2. Yes,chezea Yanga wewe.

    ReplyDelete
  3. Okwi mwisho jalinze mjini wote jaja

    ReplyDelete
  4. JAJAJAAAAAAA ndiyo habari ya mjini!!!! okwi choko tu!!

    ReplyDelete

Top Post Ad