Mama Kanumba Akanusha Tetesi za Kutoka Kimapenzi na Serengeti Boy

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mayasa Mariwata
MAMA wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa amekanusha vilivyo taarifa zilizozagaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na kijana mdogo ambaye amemzidi umri (serengeti boy).

Mama Kanumba ambaye pia amefuata nyayo za mwanaye kwa kujiingiza katika uigizaji, alifunguka hayo alipokuwa akizungumza na mwanahabari wetu mambo mbalimbali yahusuyo maisha yake binafsi na sanaa kwa jumla.

Lilipofika suala la tuhuma hizo ambazo zimewahi kuripotiwa na baadhi ya magazeti (si ya Globa Publishers Ltd) kwamba anatembea na dogodogo, mzazi huyo alisema taarifa hizo ni za kipuuzi na hazina ukweli wowote.

“Huo ni uongo tu kwa kweli, hakuna kitu kama hicho, mtu mzima kama mimi naanzaje kufanya vitendo kama hivyo? Heshima yangu itakuwa wapi?” alihoji mama Kanumba.

Mama hakusita kutoa ufafanuzi zaidi juu ya madai hayo kwenda mbele hadi kufikia hatua ya kudai kuwa anaonekana na dogodogo huyo katika maeneo tofauti.

“Wanasema nimekuwa nikionekana naye sehemu tofauti? Inawezekana akawa ni huyu mwanangu Hotma Peter ambaye nimekuwa nikishirikiana naye kwenye kazi mbalimbali kwa kuwa watu hawamjui na walizoea kuniona nikiwa na Seth Bosco (mdogo wa marehemu), ukweli sina bwana na wala sihitaji hata awe pedeshee wa aina gani,” alisema mama Kanumba.

Akizungumzia kuhusu kampuni ya Kanumba The Great Film aliyoiacha marehemu mwanaye, mzazi huyo alisema kampuni hiyo kwa sasa bado inaendeleza shughuli za filamu japo kipindi cha nyuma ilikuwa haipo bize sana kwa kuwa akili yake haikuwa sawa.

“Kampuni bado inafanya kazi, japo kwa sasa msemaji wa kampuni hiyo ni Hotma ambaye ni mtoto wa marehemu mdogo wangu, Seth kwa sasa yupo bize na mambo yake mengine japo tunashirikiana naye katika kuandaa kazi mbalimbali na tumefanikiwa kutoa filamu moja mpaka sasa.

“Ukweli ni kwamba Kanumba hakuacha kazi yoyote, kwa kuwa kazi zake zote hatimiliki walikuwa nazo Kampuni ya Steps Entertainment na ya Mtitu, ni vizuri wasanii wawe makini na hili angalau ziwepo na kampuni ambazo hazina utaratibu wa aina hiyo wa kumiliki haki zote za kazi ya msanii,” alifunguka bi mkubwa huyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wizi mtupu heri angekaa kimya tabia zake huyu mama na mama yake Lulu ni aibu tupu. Kutwa kulewa na kujiuza.

    ReplyDelete
  2. sasa uyu mama anaigiza vile ako na kipaji na yeye mana kusomea sanaa najua hajasomea ama ndio kamata fursa wabongo bwana haya twende kazi

    ReplyDelete

Top Post Ad