Shikamoo Wasanii wa Bongo, Naomba Mnijibu Maswali Yangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

1.Mimi nashindwa kuwaelewa kabisa, Hivi ni kweli nyie ni mambo safi? Yaani hela mnazo za kutosha au wanawazushia?
2.Hivi ni kweli zile picha za uchi ninazo ziona kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ni kweli au wanawasingizia?
3.Hizo nyumba ninazosikia mnajenga, wengine nasikia wanasema wananyumba nne, je ni kweli ni zenu au ni za kuzugia kibongobongo ili maisha yaende? Kama ni zenu kwanini bado mnakaa nyumba za kupanga?


4.Samahani kwa maswali yangu, nia yangu ni kutaka kutoamini watu wanayo yasema.
Kuna watu nliona na kuhakikisha wanayo yafanya ni kweli Mfano, Mhogo mchungu na Kingwendu wana nyumba kule Mbagala, Ney wa Mitego ana nyumba, Masanja joti na Mpoki, vengu, wakuvwanga wananyumba japo bado baadhi yao hawajamalizia, Madee anagari na kashanipa lifti.


Lady jay dee ana nyumba ana range ana kampuni, Juma nature ana nyumba na benz, Matonya alijengewa nabarabuu japo yeye kamalizia so ni nyumba yake ipo Tanga, Prof.Jay ana nyumba kimara na gari Mbili. Marehemu Kanumba alikua na gari, Ray wa bongo movie ana gari na Mke(chuchu hans) wanaishi pamoja sijajua kama kaoa kihalali sababu huyu mwanamke alikua mke wa mtu.


Dully sykes aka Mr Misifa anamiliki nyumba Tabata ana gari aina Honda anamiriki studio pia(Dhahabu records). Afande Sele kajenga Morogoro.

Ndugu zangu Wasanii, Kuna baadhi yenu sijui wanachokifanya.

1.Diamond nasikia ana hela yaani utajiri unao karibia billion, Kanunua Mtaa Kijitonyama Makumbusho, ana nyumba nne. Hivi haya maneno ni kweli?
Mfano juzi kati alipiga picha kwamba Kanunua V8 kumbe gari ni ya Papa Chifu Kiumbe.

Diamond ana nyumba nne lakini Mbona Mama yake Hamhamishi Pale Tandale Kila siku ya Mafuriko maji yanaingi Ndani?. Kaka Diamond anasema anahela na wasanii wengine lakini Mbona bado amepanga? Kwanini Hajakamilisha nyumba japo moja tu ahamie?

Diamond anasema ana hela, Mbona wacheza show wake Wanaishi Maisha ya dhiki kiasi kwamba kwenda makwao wanaenda kwa kujificha. Wacheza show wapo nane, kwenye hiyo billion ameshindwa kutoa hata mil 50 japo awanunulie magari used?. Anazidiwa na Nyandu tozi anayesomesha Ndugu zake sekondari karibia watoto sita.

Kaka diamond anasema Kanunua Mtaa Makumbusho, Mbona mbona akienda kwa Wema gari anapaki nje?

2.Wema Sepetu sidhani kama kweli Mambo safi, ananitia Mashaka kwa sababu Mara ya kwanza alisema amejenga nyumba Kijitonyama kumbe nyumba ni ya Mama Ngoma Mwisho wa siku akahama na sasa yupo Makumbusho. Siku za nyuma alidanganya Kanunu Gari aina ya AUDI na akawa nanipita eti hi figganigga lakini Mwisho wa siku Akaja kunyang'anywa pale Maeneo ya Namanga na Kampuni ya Majemba sababu gari ilikua ya Kaka CK(Clement huyu anayetembea na Kajala) na alikua hajamaliza kuilipia alipoinunua. Yani ile Gari Clement akua hajamaliza deni kwa mtu aliyemuuzia. Baada ya Kunyan'ganywa Diamond akasema atamnunulia V8. Hadi leo sijaona V8.

Kama Wema na Diamond wangekua na Hela wangeshindwa kulipia kipindi chao cha IN MY SHOES cha channel 5 hadi kimefungwa na Wanadaiwa bado. Kweli wana hela?

Nimetaja hawa baadhi sababu ndio Habari ya Mjini. Naomba Mniondoe ushamba wangu jamani, Hizi hela zenu wasanii Mnaosema Mnahela, Mmeziweka wapi? Au ni kipi cha maana Ambacho mumefanya. Sioni chochote zaidi ya kununua vinywaji, nguo, kuazima Magari, Majungu na Umbea. Naomba mnifafanulie hela zilipo.

Ingependeza Mtu aishi maisha yake kama Anavyo fanya B12. B12 Angarau anajitahidi ana duka pale Mwenge japo wateja sasa wamepungua sababu ya kuhamisha kituo cha basi lakini Maisha kapiga bao. Hana nyodo anatoa hai kwa washikaji. Nia yangu ujirudi kwa sababu umri unaenda na dogo kashaanza shule.

Nyie Bongo Movie Hela zenu zipo wapi? Watu wanashindwa hata kuwasaidia sababu wanajua Mnahela kumbe weupe.
Nawapenda Sana ndugu zangu. Mia

Written By figganigga Via JF
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. pumba tupuuuuuuu,unachuki binafsi malaya wewe fanya yako,Diamond na Wema are forever paka shume wewe mtasema mengiiiiii,lofa mmoja weweee wivu tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtazamo wake tu achana nae........

      Delete
    2. KAMA KWELI MNAMPENDA NA KUMSHABIKIA MUAMBIENI UKWELI, MAANA ANGEPOTEZA MAISHA UJERUMANI KWA AJILI YA LAKI 5, ALAF DEM WAKE ANAGAWA PESA JAMAA ANAZOTAABIKA NAMNA HIYO, SASA NYIE WASHABIKI SI NDO MNGETAFUTA NAMNA YA KUMSADIA KUTUMIA PESA WISELY. ACHENI UPUMBAV NA ANGEULIWA MNGEMSHABIKIA NANI??N

      Delete
  2. Mijitu bongo Ina Wivuuuuuuu mpaka inakera.mtaishia kuwa malofa mpaka mnaingia kaburini

    ReplyDelete
  3. ..SINA ISSUE NA YEYOTE ILA NAFIKIRIA TU, KUNA SIKU NIMESOMA DOMO KATAKA KUULIWA UJERUMANI ALAF NIKAMUONA MADAM ANA M SHOWER MWIMBAJI WA BENDI FLAN NASIKIA NA KITU KAMA BOX 1 HIVI NA JAMAA ALITAKA KUPOTEZEWA UHAI KWA EURO 250 KAMA LAKI 5 HIVI SASA HAPO NAFIKIRI NDO ELA ZINAPOISHIA, COMMON SENSE LAZIMA ITUMIKE ELSE ITS JUST A MATER OF TIME.

    ReplyDelete
  4. Waacheni watu na maisha yao yanawahusu nn km kweli unataka kutoa somo kw awote kwann uelemee upande wa daimond tu hizo ni chuki zetu binafsi kwakweli na hata hivyo hayakuhusu na uclolijua ni sawa na ucku wa giza pukuta matako tembea na YESU

    ReplyDelete

Top Post Ad