Joyce Kiria Akwaa Skendo ya Utapeli ya ile ya Biashara ya Telexfree

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Why Joyce? Hosti wa Kipindi cha Wanawake Live kupita Televisheni ya EATV, Joyce Kiria yupo kwenye wakati mgumu baada ya kukwaa skendo ya utapeli kwa marafiki zake (majina yanahifadhiwa kwa sasa) akidaiwa kuwashawishi kuingia kwenye biashara ya Mtandao ya Telexfree Network Marketing.

Kwa mujibu wa sosi makini, ishu hiyo imeibuka juzikati ambapo Joyce alikuwa akishushiwa zigo la lawama na marafiki zake hao huku baadhi wakitishia kumshitaki kwa kuwatapeli kwani wamepoteza fedha nyingi kwenye mpango huo wakidai hawajaona chochote.

“Dada Joyce aliwashawishi marafiki zake wengi, wakaingia na kila watu walipomshtua na kumwambia kuwa ni utapeli mtupu alikuwa akiwatolea lugha za kuudhi. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Joyce na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alifunguka: “Ni kweli niliwashawishi marafiki zangu kwa sababu nilijua biashara hiyo inalipa na hata mimi nimeumia sana kuona imekufa kwani sikupenda.

“Nimepoteza fedha nyingi. Ilikuwa ni kama desi ilivyokufa, hakuna wa kulaumiwa.”
Joyce aliongeza kwamba, kama kuna watu ambao wanadai amewatapeli waende mahakamani kwa sababu hakuwalazimisha kuingia wala hakuwashikia panga.

Telexfree Network Marketing ni kampuni iliyokuwa ikijihusisha na biashara ya mtandao ambapo mhusika hutoa kiasi cha fedha huku akiunganisha watu wengine ambapo kipato chake kwa maana ya faida itaongezeka mara kwa mara kwa kadiri anavyounganisha watu wengi.
Credits:Globalpublishers
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad