Godbless Lema asema atangaza kuwania ubunge Kinondoni uchaguzi wa Octoba 2015

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katika kikao chake na waandishi wa habari mchana huu katika hotel ya Snowcrest jijini Arusha, Lema amesema anaenda kupambana na Iddi Azan kwenye jimbo la Kinondoni ktk uchaguzi mkuu ujao mwezi October mwaka huu. Akielezea nia yake hiyo mbele ya mamia ya waandishi wa habari, Lema amesema anataka kuleta mapinduzi ya fikra kwa wana kinondoni na kuijenga ngome imara ya chadema jimboni hapo. Alisema mpango wake huo alikuwa nao toka mwaka 2013 pale alipovuliwa ubunge na alitafakari kujiingiza kwenye changamoto mpya kisiasa ifikapo mwaka 2015.

"Wana wa Arusha wasiwe wanyonge, kamanda wao naenda kupambana kwenye uwanja mwingine wa vita lakin wajue tupo pamoja" Alinukuliwa akisema bw. Lema. Hata hivyo alikwepa kujibu swali la mwandishi wa Radio 5 aliyetaka kujua kama pengine ni mbinu ya Lema kukwepa aibu ya kushindwa kwenye uchaguzi huu ikizingatiwa historia yake tata ya utekelezaji wa ahadi zake alizotoa mwaka 2010 na pia ushindani mkali unaomkabili ndani ya chama chake. Imefahamika kuwa wanachama zaidi ya 30 wameshatangaza waziwazi kuchuana na Lema kwenye uchaguzi wa Octoba.
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya Lema kukimbia changamoto na kujaribu karata yake mahali pengine
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alijua moto unaokuja ndani ya chadema tulijipanga tunataka watu wa vitendo sio longolongo. Kaharibu sana chama chetu hata vikao na wananchi hakuna tokea achaguliwe hakuna hata ahadi moja aliyotekeleza , Joshua Nasari kwa muda mfupi kafanya mambo mengi sana.
    Shida ya Lema ni mtu wa jukwaa tu vitendo hana kabisa na anapenda tu kupita na kusifiwa na vijana kuwa ni kamanda wa fujo.

    ReplyDelete

Top Post Ad