Madai ya Kubeba Unga: Ray C Ajisalimisha Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya kukiri kwa mdomo wake kutumia madawa ya kulevya ‘unga’ na baadaye ‘kustaafu’, madawa hayohayo yamemletea msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ ‘msala’ ambao umemfanya yeye mwenyewe, kwa hiyari yake ajisalimishe polisi.

Hivi karibuni, Ray C alijikuta akiangua kilio ndani ya Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar baada ya kuhusishwa na ishu ya uuzaji wa unga.

Chanzo hicho kilinyetisha kwamba, siku ya tukio, wakati Ray C akitokea nyumbani kwake, alipofika maeneo ya Kawe Darajani aliona pikipiki ikimfukuzia na baadaye ikampita na ‘kumbloku’.

Ilisemekana kwamba baada ya kusimama, jamaa alishuka kwenye pikipiki kisha akamwambia aegeshe pembeni gari lake aina ya Toyota Carina TI.

Chanzo kilidai kwamba, Ray C alikataa kufanya hivyo kwa kuhisi aliyekuwa akimwamrisha ni jambazi.

“Ray C aliamua kuondoa gari kwa kulazimisha ambapo alimkwepa jamaa huyo kisha kukanyaga mafuta ambapo gari liliondoka kwa kasi,” alisema.

Ilisemekana kwamba baada ya kufika kwenye kituo cha daladala cha Lugalo, alisimama na jamaa huyo aliyekuwa akimfukuzia akaegesha pikipiki mbele yake na kumtaka Ray C ashuke ndani ya gari kwani alitaka kulipekua akimwambia kuwa alikuwa amebeba unga.

Ishu hiyo ilizidi kumtia Ray C wasiwasi na kumuuliza jamaa huyo ni nani ambapo alisema kuwa yeye ni askari.

Kwa kuwa hakuwa na sare, Ray C hakuamini jambo lililosababisha jamaa huyo kumuonesha kitambulisho kilichokuwa kimechakaa.

Baada ya kuona hivyo, Ray C alimwambia waongozane hadi Kituo cha Polisi cha Oysterbay lakini jamaa huyo alikataa na kumtaka waende Kawe jambo ambalo Ray C alishindwa kuafikiana nalo na kuondoa gari lake akimwambia waambatane hadi Kituo Kidogo cha Polisi cha Mwenge.

Jamaa huyo alionekana kutotaka kwenda hivyo Ray C aliondoa gari kwa kasi na kuelekea Mwenge ambako alikuwa akiomba msaada kwa matrafiki na alipoona wanachelewa aliondoa gari kumkimbia jamaa huyo.

Ilisemekana kwamba awali alitaka kukimbilia Kituo cha Polisi cha Mwenge lakini alipoona kuna msongamano alikimbia kwenda kujisalimisha Mabatini huku akiangua kilio.

Baada ya kushibishwa taarifa hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Ray C ambaye alielezea mkasa mzima.

Alifunguka: “Ni kweli ulivyoambiwa tulitoka Lugalo na kuelekea Mwenge baada ya kufika kwenye makutano ya Mwenge niliwaona askari wawili na trafiki akiwa pembeni, nikawasimamisha na kuwaeleza.

“Askari mmoja alikubali kupanda kwenye gari langu nikaenda naye hadi Mabatini.

“Baada ya kufika Mabatini nilieleza kila kitu kwa mkuu wa kituo hivyo akaniambia nisiwe na wasiwasi.

“Bada ya hapo mkuu wa kituo aliita askari wa kike na wa kiume nikaongozana nao hadi katika gari langu na kupekua kila sehemu lakini wakasema hapakuwa na chochote kibovu, hivyo nikawa nalia tu na mkuu wa kituo akaniomba ninyamaze na kuniruhusu nikaondoka zangu kwenda Hospitali ya Mwananyamala kumeza dawa."

Credit: Gpl
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kazi kweli kweli ndiyo mshara wa tabia uliyokuwa nayo.pole sana

    ReplyDelete
  2. Huyu naye anatafuta sana attention ya watu. Time yako ilishaisha

    ReplyDelete
  3. Huyu naye anataka sana attention ya watu. Mara panya road, mara dengue mzushi tu huna lolote ndugu kubali tu kwamba ulishafulia

    ReplyDelete

Top Post Ad