Mwanasheria Albert Msando Afunguka kuhusu Kufukuzwa Zitto Kabwe Chadema


Mwanasheria ambaye pia ni diwani kupitia CHADEMA, Ndugu Albert Msando amehoji yafuatayo;

1. Amehoji je, kama CHADEMA kinasema ni Cha Kidemokrasia kwanini kinaaamuru Afukuzwe tu kwa kuwa ameenda mahakamani?

2. Amehoji je, ni nani mwenye mandate ya kumvua mwanachama uanachama wake.

3. Je, uamuzi wa kumvua uanachama ulipaswa kutangulia kwa umma au kwa Zitto kwanza?

4. Amehoji je, imekuwaje mtu anayesimamia sakata la Escrow afukuzwe kwa sasa?

5. Amesema pia kuwa Zitto hana haja ya kubaki CHADEMA kwa kuwa hata akiomba kubaki haitakuwa na mashiko. Pia ameuliza itakuwaje akae meza moja na Tundu Lissu,Wakati Tundu Lissu anatangaza amesema walishamfukuza toka mwaka jana. Naye anaona kuwa Zitto hahitajiki CHADEMA.

6. Pia amesema lengo la kumfukuza Zitto limefanywa kinafiki tu.

7. Amesema kuwa haoni haja ya kulazimisha kila mtu awaze kama Tundu Lissu au Mbowe au Slaa.

9. Pia amesema kuwa mgogoro huu ni funzo kwa Zitto, Wanachadema na Watanzania kujua aina ya viongozi walionao.Pia amesema kuwa migogoro hii isitumike kujenga chuki.

Chanzo: Clouds TV

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CHADEMA BYE-BYE,CUF KARIBUNI KUPAMBANA NA CCMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMMM

    ReplyDelete
    Replies
    1. CHADEMA CHAMA MAKINI HAKUNA KULINDANA KAMA CCM

      Delete
  2. NDIO NI FUNZO KWA WOTE

    ReplyDelete
  3. CHADEMA WANATAKIWA KUWA MAKINI SANA HUO NI MWANZO WA KUCHAFUA CHAMA CHAO...POLE

    ReplyDelete
    Replies
    1. NI CHAMA MAKINI HAKUNA KULINDANA PEOPLES POWER
      .

      Delete
  4. Watanzania sie ni watu wa ajabu sana! Kutenda haki si jambo rahisi inataka ukomavu wa hali ya juu! Kila siku tunalalamika kuwa hapa nchini haki haitendeki ikitokea watu wakatenda haki tunalalamika tena! tutafika kweli

    ReplyDelete
  5. PEOPLES POWER CHADEMA HAKUNA KULINDANA!!!!!!!!!!! HONGERENI SANA

    ReplyDelete
  6. Nani kasema zitto ni mpinzani? Alikua mpinzani kwenye term yake ya kwanza ya ubunge aliporudi bungeni kwa Mara yapili alikua pandikizi la CCM zitto sasa hivi sio mwanasiasa anapiga deal acha akusanye wajinga wake apige hela Chama gani cha upinzani kimeshawahi tokea Tanzania kikawa strong Kama chadema. Leo hii zito Kabwe anakihujumu Chama sababu ya tamaa ya fedha badala angetulia na wenzake yeye anaenda kukata buti tena? Kama zitto asungekua msaliti akawa kitu Kimoja na wenzake huko chadema kitu gani kingewazuia chadema kuchukua nchi kwenye uchaguzi ujao? Huyu ni yuda

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad