Hukumu ya Kesi ya Mwanamuziki Lady Jay Dee Kuichafua Clouds FM Yatolewa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye ile kesi ya kudaiwa kuuchafua uongozi wa Clouds Media Group na mkurugenzi wake wa vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba iliyokuwa ikimkabili staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ imetolewa hukumu ambapo mwanamuziki huyo ameamriwa kutozungumza chochote (amefungwa mdomo) juu ya walalamikaji hao.

Habari za kuaminika kutoka kwenye chanzo makini zilidai kwamba hukumu ya kesi hiyo juu ya malumbano yaliyokuwa makali kati ya pande hizo, ilikamilika hivi karibuni ambapo Jide au Lady Jaydee alipewa maelekezo hayo.

Ilidaiwa kwamba staa huyo alielezwa kuwa endapo atakwenda kinyume na hukumu hiyo atakuwa amepingana na amri ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo.


“Kesi ilikuwa ikirindima kwa muda mrefu kwenye mahakama hiyo lakini hivi karibuni imefikikia tamati,” kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimtafuta Ruge ili kuthibitisha habari hiyo ambapo alikuwa na haya ya kusema:

“Ni kweli kesi moja ya kututukana kwenye mitandao ya kijamii imeshatolewa hukumu na kwa taarifa ni kweli hatakiwi kuongea chochote juu yetu ila bado kuna kesi nyingine inaendelea, nafikiri maelezo mazuri zaidi nitakukutanisha na wakili wetu ndiye atakufafanulia zaidi.”

Mei, 2013, Clouds Media Group na Ruge walimburuza Jide mahakamani kwa kile walichodai kwamba alikuwa akiwatukana kwenye mitandao ya kijamii.

GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad