Jini Kabula Afakamia ‘Mikuku’ Uwanjani!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jini Kabula
Staa wa Bongo Movies, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ juzikati alinaswa akifakamia minofu ya kuku katika ya kadamnasi iliyojitokeza katika Dimba la Taifa jijini Dar.

Tukio hilo lilinaswa Machi 17, mwaka huu ndani ya uwanja ambapo kulikuwa na mtanange kati ya Yanga na Kagera Sugar.

Akiwa uwanjani hapo muda mfupi kabla ya mechi kuanza, Jini Kabula alishuhudiwa akifakamia ‘mikuku’ na rafiki zake, jambo lililowafanya baadhi ya mashabiki wanaomfahamu kumkodolea macho muda mwingi.

Pamoja na hali hiyo, Kabula hakuonekana kujali chochote akaendelea kutafuna kuku kwa fujo na hata mwanahabari wetu alipomhoji juu ya upatikanaji wa kuku hao ndani ya uwanja huo, staa huyo alisema kuwa aliwanunua nje ya uwanja hivyo hata kula katikati ya watu haoni noma.

“Acha nile kwa raha zangu, mimi nina njaa na ndiyo maana nilipitia kuku wangu nje ya uwanja na kuja nao hapa,” alisema Kabula.

GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad