Sakata la Urais, January Makamba Amlipua Lowassa, Soma Alichokiandika

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

January Makamba
January Makamba Amfungukia Lowassa.....Soma Hapa Chini:

"Nafasi ya Urais ni nafasi ya hadhi na heshima kubwa. Unapoiomba hupaswi kufanya michezo ya kuigiza. Huu utaratibu wa kuratibu watu, kuwasafirisha, kuwapa posho na ubwabwa waje kukuomba kugombea ni michezo ya kuigiza ambayo ni aibu kubwa.
Kila mgombea ana uwezo wa kutengeneza WATU wa kumuomba kugombea lakini wengine hatufanyi hivi kwasababu tunaheshimu nafasi tunayoiomba na tunaamini kwamba haipaswi kutafutwa kwa ulaghai na maigizo.

Ni aibu sana kutumia shida na njaa za watu kisiasa. Ni aibu sana kukusanya vijana na wazee wa watu na kuwapangia viti na mahema na kuwapa pesa halafu pesa na kuwapiga picha. Ukiona mtu anatafuta nafasi ya uongozi kwa ujanja na ulaghai ujue atatawala kwa ujanja na ulaghai.
Viongozi wanaokubalika na watu hawangaiki kupanga Viti na mahema na kuwapiga picha watu wanaowakubali.

Mgombea anayehaha na kutumia pesa nyingi kuonyesha anakubalika ukweli ni kwamba hajiamini. Kama unakubalika huwezi kuratibu makundi na kuyalipa na kuwapiga picha na kuita waandishi wa habari waje kushuhudia. Hizo ni mbinu za mfa maji.

Naamini Chama changu hakitatishwa na nguvu za maigizo. Tunataka uongozi safi unaomuogopa mungu. Tunataka uongozi wenye uadilifu na fikra mpya za kuisogeza mbele Tanzania. Tunataka viongozi watakaomaliza shida za Watanzania sio wanaozitumia shida hizo kisiasa
Hata Mzee Makamba, pamoja na umri wake wa miaka 75, leo akiwa na pesa za kumwaga anaweza kutengeneza makundi yakamuombe kugombea Urais.

Ifike mahali katika nchi yetu tuache hii michezo. Tukiendelea na mambo haya, tunatengeneza taifa linaloendeshwa kwa propaganda tu. Watu wanaotaka kuomba nafasi ya Urais wanapaswa kuwa na ujasiri na wanapaswa kujiamini na kusema wanataka nafasi hiyo na wana fikra gani mpya bila kutumia pesa kuonyesha kwamba wanagombea kwasababu wanahitajika na watu. Uongozi thabiti na shupavu hautokani na michezo ya kuigiza."
January Makamba.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ulichokinena ni kweli kabisaaaa...lkn pia tuna mashaka pamoja na chama chako hakitufai kabisaaaa....miaka mingapi ss muko madarakani na hkuna zaidi ya kujaza matumbo yenu tuuu.......ss tunasema ....TUMECHOKAAAAAAA....NARUDIA TENA TUMEWACHOKAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  2. Wote wezi nyie mnajuana vizuri.

    ReplyDelete
  3. Kayaongee hayohayo kwenye kupitishanakwenu huko Chimwaga tukusikie,si utakuwemo!

    ReplyDelete
  4. CCM Mkafie mbeleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  5. ..we DOGO Januari hata wewe hujiamini ndiyo maana yanakutoka hayo. Kale kakitabu kako ulikoandika kalikuwa na maana gani kama si kujifagilia tu. Kiongozi mzuri anasifiwa na watu na asiye mzuri anajisifia mwenyewe.kama wewe. Kiongozi BORA kama EDDY anapata heshima lakini kiongozi BOMU kama WEWE anadai kupewa heshima.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa hapo juu at 7:51 PM swadakta umenena jambo yaani point tupu take 5

    ReplyDelete
  7. Lowasa hawezi kuwa kiongozi bora. Bora tutawaliwe na Kiongozi MWANAMKE kuliko Lowasa,, Ndio walewale!

    ReplyDelete
  8. Umesema mambo ya msingi kabisa.

    ReplyDelete
  9. marefarii hawaongozwi na wachezaji

    ReplyDelete
  10. Kajambe mbeleeeeee!!!!!

    ReplyDelete
  11. we anony wa hapo juu unachekesha! eti bora tutawaliwe na kiongozi mwanamke kuliko lowasa, kwa nini umemtumia mwanamke kwa namna hiyo? kwani wanawake hawawezi uongozi?

    ReplyDelete
  12. umefikaje hapo wewe kama si kubebwa tuu. Unapopataka pana kamwendo dogo na ujue Mungu akisema ndio hata watu wasemeje watasema bure kama ninafasi yake ni yake tuu. Cthani kama mtu kama Lowasa anaweza aka organise watu kiasi hiki hasa viongozi wa dini wa kipentecost c angefanya kwa wa Lutheri anakosari yeye. Ni Nyota yake tuu watu wanajua anaweza akafanya jambo likaonekana na ndio mtu wanamuhitaji kwa sasa. Wewe endelea na ku compile vitabu sijui ni report au????

    ReplyDelete
  13. WEWE UWE RAIS????? BANDARI ITAHAMIA MOROGORO

    ReplyDelete

Top Post Ad