Vita ya Ray C na Zamaradi Yapamba Moto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zamaradi na Ray C
Wale Mastaa waliodaiwa kuingia kwenye bifu zito, Zamaradi pamoja na Ray C, na baadae kupatana, huku chanzo cha bifu kikidaiwa kuwa ni mwanaume, bifu hilo limeibuka tena, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni maneno ya kejeli ya mtangazaji zamaradi mketema kwa mwanamuziki Ray C.

Hivi karibuni Zamaradi aliposti picha ya mwanae kwenye mtandao wa Instagram akim wish Happy birthday, uku aki repost baadhi ya pongezi kutoka kwa baadhi ya mastaa na mashabiki mbali mbali wa mtangazaji huyo, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuwa mwiba kwa mwanamuziki Ray C ambaye mpaka sasa hajabahatika kupata mtoto.

Mtangazaji huyo ambaye baadae tena aliandika comment kwenye page yake, akiwauliza mashabiki wake ni kitu gani ambacho wanatamani kuwa nacho katika maisha lakini hawana? Au wengine wanavyo na vinawafanya wawe na furaha?

Comment hiyo ilizua utata uku baadhi ya wadau wakidai lile lilikuwa dongo kwa hasimu wake wa mda mrefu ray c ambaye mpaka sasa hajabahatika kupata mtoto wala kuolewa, ndipo team Ray C ilipoamua kumtag boss wao huyo ambapo Ray C hakutaka kulaza damu na kuamua kujibu mapigo kwa mtindo ule ule wa vijembe, hali iliyozua balaa uko Instagram na kuziacha team hizo mbili zikishambuliana kwa matusi ya nguoni.
“Bitchez be like (Marry Me can't u see am pregnant again)????????(Players be like(In your Dreams keep popping dem kids!!!!)lol!”-Ray C aliandika

Ray C baada ya kuona hali inakuwa mbaya, alihoji kama Zamaradi ndiye mwanamke pekee aliyezalishwa bila kuolewa apa duniani? Aliwataka watu waache kuhisi vitu ambavyo hawana uhakika navyo.
Mpaka sasa bado Zamaradi ambae siku ya jana amejifungua motto wa pili hajazungumza chochote kuhusu varangati hilo.
By Warumi-on JF
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu Zamaradi naye anajizalia watoto haraka haraka kwa fujo ili aolewe, anadhani mwanaume kama anakupenda uje mke wake ni lazima ukimbilie kuzaa kabla ya ndoa? Kama anakupenda kweli atakuoa hata kama hajakuzalisha, watoto ni majaaliwa, sasa yeye anazaa usiku na mchana anadhani ni sifa au watu wataona anapendwa sana, anajidanganya na kujizeesha bure, yeye anakazana kuzaa na kulea, wenzie wanakula bata na bwana usiku na mchana, na mbaya zaidi bwana mwenyewe bado yupo yupo sana hana mpango wa kuoa leo wala kesho kwa madai kwamba bado hajampata wa kumpa nafasi ya kuwe mke wa ndoa. Hapo sasa!!!!

    ReplyDelete
  2. KHA!!!!!!! RUGE KUMBE NAWE MHARIBIFU!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad