Taasisi Ya Kiislam Yaitaka Serikali Iwakamate Maaskofu Waliotoa Tamko...Yasema Wasipokamatwa Itahamasisha Waislam Wote Kupiga Kura Ya HAPANA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Taasisi ya dini ya Kiislam imeitaka serikali kuwakamata maaskofu na wachungaji ambao  inadai wametoa matamko ya kichochezi na endapo serikali itashindwa kuwakamata, basi jumuiya hiyo itawahamasisha waamini wa dini ya kiislam popote walipo kuipigia kura yaHapana Katiba inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
 
Kauli ya taasisi hiyo yenye misimamo mikali inatokana na Tamko lililotolewa  na muunganiko wa jumuiya ya Kikristo,ikiwemo Baraza la Maaskofu katoliki (TEC),Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT)  na  Baraza la Makanisa la kipentekoste(CPCT) ambao wote  kwa pamoja waliwataka waumini wa dini ya kikristo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba inayopendekezwa kutokana na serikali  kuruhusu mahakama ya Kadhi kisheria.
 
Akitoa tamko la Taasisi ya Dini ya Kiislam  ambalo ni muunganiko wa taasisi za dini hiyo zaidi ya 11 hapa nchini,Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh Rajab Katimba wakati wa Mkutano na Vyombo mbalimbali vya habari  jana  Jijini Dar es Salaam, aliitaka serikali kuwachukulia  hatua maaskofu hao kwa madai ya kufanya uchochezi.
 
“Serikali iwachukulie hatua za kisheri maaskofu na wachungaji kwa kutoa matamko yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia ya kidini kwa waislam kinyume cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.
  
"Tunataka  Maaskofu  hao  wakamatwe,wafikishwe mahakamani na  dhamana  izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali,lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwaalisema Seikh Katimba.
 
Aidha, Sheikh Katimba  aliitaka  Serikali kuendelea na Mchakato wa uundwaji mahakama ya kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya kamati ya sheria na utawala wa bunge kwa kuzingatia mambo muhimu  mawili.
 
Mosi: Serikali iache njama na hila za kuigeuza mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA na MUFTI wa BAKWATA.
 
“Endapo serikali itaendelea na kuwasilisha muswaada wa Mahakama ya Kadhi unaoipa mamlaka Bakwata kuunda,kusimamia,kuteua makadhi nakadhalika kinyume na maoni ya Waislam wengi itakuwa imethibitisha kuwa serikali haikuwa na nia ya kweli ya kuunda na kuanzisha mahakama ya Kadhi alisema Sheikh Katimba.
 
Pili: Serikali igharamie mahakama hiyo kama inavyogharimia uendeshaji wa mashauri yaliyopo kwenye mahakama za kawaida yanayohusu sheria za kiislam ambayo mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa.
 

Na pia mahakama  hiyo igharamiwe na serikali  kama inavyogaramia huduma za makanisa chini ya mkataba maarufu uitwao memorandum of understanding (MOU) , mkataba  ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya waislam” alisema  sheikh  huyo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtasugua gaga kama mnasubiri wakamatwe kwanza wataanzia wapi kwa mfano

    ReplyDelete
  2. Mtasugua gaga kama mnasubiri wakamatwe kwanza wataanzia wapi kwa mfano hebu waanze tuone

    ReplyDelete
  3. Mtasugua gaga kama mnasubiri wakamatwe kwanza wataanzia wapi kwa mfano hebu waanze tuone

    ReplyDelete
  4. Hawa ndo kabisa wameharibu, hawajui kitugani wanataka. Kwanza wao lazima wakubaliane kwamba wako chini ya BAKWATA!

    ReplyDelete
  5. Mungu wetu iponye Tanzania tusaidie huku tunako elekea siko katiba inatusaidia wote inatengenezwa kwa manufaa ya kila mtu sio mtu moja unaposema wa kamatwe wamefanya nini wamekosea wapi lazima mtu anapopewa katiba aelwe nini anatakiwa afanye Mungu awape ufahamu msilete sababu zisizokuwa za msingi ambazo hazijengi nyie ndo mnaleta uchochezi mnaosema wakamatwe kwa kosa gani hebu Mungu awafungue ufahamu wenu muelewe hatuonyeshi nguvu kila mtanzania anatakiwa aelewe sio ugonvi Mungu awasaidie sana katika hilo

    ReplyDelete
  6. Wenyewe hawajielewi.

    ReplyDelete
  7. Bakwata haitakuwa na fedha za kuendesha Mahakama za Kadhi ambazo huwa na makadhi (mahakimu) wanaohitaji mishahara kila mwezi. Serikali inapaswa kuzihudumia hizo mahakama. Mbona Serikali inahudumia Ukiristo kwa muda mrefu sasa? Serikali ikikataa kubeba hizo gharama itakuwa ni ubaguzi wa wazi na utaigharimu serikali.

    ReplyDelete
  8. Jamani ni taasisi ipi ya ki kristo inahudumiwa na selikali?taasisi zote za ki kristo zilikuwa zinapata misaada kutoka nje.kwa sasa taasisi hizi zinamifuko yake ya hifadhi.selikali yetu haina dini jamani hivyo tusiibebeshe mizigo isiyokuwa yake.

    ReplyDelete
  9. Anonymous wa 8:39 AM wewe ni pimbi kabisa, tena nimeamini waislamu wote ni wapumbavu wa akili, toa mfano wa namna gani serikali nahudumia ukristu? yaani madini mengine haya ya kishetani ni hatari kabisa, wewe unafikiri hapa ni iran, ninyi waislamu huwa ni majinga sana, mmejinyanyasa wenyewe kwa muda mrefu sana kisaikolojia kwa kuendekeza mishule yenu hyo ya madrasa leo mmestuka muda umeshawatupa mkono, jitoe mianga basi kama wafanyavyo nigeria na kwingineko, shenzi taipu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anonymous wa 10:39, dini ya kishetani ya mamaako na babaako!toa point acha kutukana dini za watu,shenzi ww na ndugu zako midivishen five utaijua tu,paka shume wewe

      Delete
    2. ndio maana mnaoana makanisani..dini ya mashoga na malaya

      Delete
    3. ULAANIWE KABISA WEWE,NI DINI GANI AU UKRISTU GANI UNAKUAMURU KUTUKANA DINI YA MTU?TUBU!

      Delete
  10. Anonymous wa 8:39 wewe wa hapo juu kuwa na busara na maneno unayoyatoa sio utukane watu na dini zao .weka maneno ya msingi na sio kukurupuka tu kwa jazba

    ReplyDelete
  11. wewe mwenye kutukana dini za wenzio..hivi unamaana gani ..eti tumestuka muda umeisha kwisha???wewe uliyestuka zamani mbona unaelekea kiuenda wazimu..ungekuwa mwenye akili timamu usingetoa comment utumbo kama.hii..hakika sisi hatukufahamu na hatukuoni..Lakini Mola Muweza ndo Anayekuona..na kama ni kweli wewe ni mkristo safi..sasa mbona unatukana hivyo wanadamu wenziwe.?..hii unasababisha vurugu..hope unajuwa vita haina macho..na wakiamua kujiripuaa itaanzia kwako..maana wewe na wenzio kama wewe ndo chanzo cha vurugu..Acha hizo muabudu Mola wako..siku ya siku..utaMface na Atakuuliza Ulikuwa unaandika comments za namna gani?

    ReplyDelete
  12. Jamani tupendane wote ni wa mungu,kwa uwezo wa kristo yesu tutashinda na kuwa wamoja.tumsifu yesu kristo

    ReplyDelete

Top Post Ad