Alichokiongea Profesa Muhongo LEO Wakati Akitangaza Nia Yake ya Kugombea Urais Kwa Tiketi ya CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

1.Niko mbele yenu sio kufanya kampeni ya urais, niko mbele yenu kuomba ridhaa ya yenu kugombea nafasi ya urais muda ukifika.
 
2. Siko hapa kumlaumu mtu au ukimshambulia kwa sababu ukimlaumu mtu umAsikini bado uko palepale. Nikisema historia yangu yote muda hautatosha, kisomo nimesoma mpaka mwisho wa kusoma, kama ni taalumu nimefikia mwisho.
 
3.Nimepata bahati ya kusoma vyuo vikubwa sana duniani na sehemu kubwa nimepatia Ujerumani ndio maana wengine wanasema nafanya kazi kijerumani.

4. Nimefanya utafiti kwa miaka 30,chama cha majiologia wamerekani kilichoanza mwaka 1988, mimi niko ngazi ya juu pia kwa waingereza na wachina niko ngazi ya juu kabisa.

5.Kwenye uasisi mwaka 1976, CCM inaanza 77 sisi ndo waasisi, kadi hii hapa. Kama nimeweza kutunza kadi ya CCM tangu 75 basi mimi ndio naweza kutunza rasilimali zenu.

6.Toka tunapata uhuru tuna vikwazo, ujinga, maradhi na umasikini Mwl alitueleza. Nil lazima matatizo yatakuwepo kwenye jamii.

7.Rushwa kubwa na ndogo, ukosefu wa ajira, siasa imekwenda kila mahala, taifa linanyemelewa na uvuvu na utegemezi, dhulma, upungufu wa upatikanaji wa takwimu sahihi, tumepungukiwa ushindani kama taifa, tumeshindwa kujiamini.
 
8. Haya ndio nataka kuyashughulikia mimi. Upungufu wa mshikamano wa taifa letu. Kwetu asilimia 51 waislamu na 49 wakristo hivyo matatizo ya madhehebu hapa ndipo mahala pake. Afrika ina nchi 54, mimi nimeeenda 52 kasoro Mauritania na Chad. Ningekua sio muaminifu nisingepokelewa huko, ulaya nimezunguka.

9.Lazima Tujue hali halisi ya uchumi wetu, chukueni kalamu na karatasi. Lazima useme unatoka wapi unaenda wapi! India asilimia 74 wanajua kusoma na kuandika. Nchi inayoongoza kwa watafiti ni Finland.(Anataja takwimu za nchi ambazo tulikuwa tunafanana uchumi baada ya vita ya pili ya dunia ikiwemo India, Brazil, China na Kenya.) Sipendi sana kujilinganisha na Kenya kwa sababu sote ni maskini.

10.Dira ya maendeleo inasema miaka kumi kutoka sasa Tanzania isiwe nchi masikini, tusikae pembeni, tusogee juu kidogo. Hakuna mwenye uwezo huo ni mimi tu ili tufikie pato la dola bilioni 200 kutoka dila bilioni 40. Mwaka 2025 tutakuwa milioni 60, nataka tule miogo na viazi kwa hamu na sio kwa shida.

11.Siwezi kukupa ahadi ya mishahara wakati sijakuza uchumi, siwezi kukupa ahadi ya kukujengea shule wakati sijakuza uchumi, tukuze kwanza uchumi.

12.Naombeni ridhaa yenu nisimamishe deni la taifa lisiongezeke, mwenye dawa ya umaskini ndani ya CCM, CHADEMA, NCCR ni profesa Muhongo tu. Elimu kuiboresha lazima tuongeze bajeti, haiwezekani darasa limerundikana ukafundisha. Anaeweza ni mimi tu sababu wengine utafiti wanausoma kwenye magazeti tu.

13.Wana CCM mnae mwanasayansi wa dunia, si mnipe tu! Tutatumia rasimali, madini yetu tumeyachimba kwa asilimia 10 kitu, mimi ndio nimetengeneza ramani ya madini ya Tanzania, Africa na duniani nikiwa vice president. Nilizunguka hii nchi kuchora ramani ya madini kwa uzalendo, ningiweza kuja na ramani na kuuzia serikali.

14. Mimi mtu anidanganyi, unakuja tunajadiliana, hii sio dunia ya kuandikiwa tu, inabidi na wewe ujiandikie. Niliweka mipango ya kuwapunguzia bei ya umeme. Ilibidi nitoke kidogo mpate machungu mnichague.
 
15. Nawaomba ifike mahala ifike mahala tuachane na matumizi ya kuni na mkaa, ni aibu sana. Tutajenga mabomba nchi nzima gesi itumike majumbani. Kila nyumba iwe na mabomba mawili, la maji na la gesi.

16.Wengine mnaweza kuwadanganya, mimi hamuwezi kunidanganya, gesi yenu ipo kwenye mikono ya uhakika kwa professa Muhongo tangu nimeanza kusoma wakati niko chuo kikuu cha Dar es Salaam na nimefanya maisha yangu yote.

17.Mapato ya gesi yasiende hazina, tutafungua mfuko maalumu na bunge litakua linaizinisha asilimia ngapi iende kwenye bajeti. Mtanzania yoyote asiwe na maamuzi ya kutumia hizo fedha bila idhini ya watanzania.

18.Mimi sipendi wawekezaji wababaishaji na si kwamba sipendi wawekezaji wa ndani, haya yote ya ujenzi wa uchumi lazima tuwe na umeme. Na umeme wa bei nafuu ndio kazi niliyokuwa naianza. Umeme ulikuwa haukatiki mara kwa mara, muda umefika tusijidharau, lazima tushinde.

19.Lazima watanzania zaidi ya asilimia zaidi ya 75 wawe wanatumia umeme, tutatumia vyanzo vyote vya umeme. Lazima mtembee kifua mbele professa Muhongo amitimiza ahadi ya CCM, hata ilani mpya inayokuja mtekelezaji atakaetekeleza kwa uhakika ni professa.

20.Ni lazima tupambane na rushwa, na sio maneno kupambana nazo na nyie wananchi muwe na uelewa na haki zetu. Mnaombwa rushwa kwa sababu hamjui haki zenu. Naomba ridhaa yenu mniteue niwe mgombea wenu. Wakulima na wafugani ni mwisho wa kuuana chini ya prof Muhongo, tatizo sio ardhi, ni technologia.

21.Uwezo ninao, maarifa ninayo, jinsi ya kutafuta fedha ndani na nje, ambacho sina ni nyinyi kuniteua tu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad