Membe: Nikiwa Rais Wasanii Wataenda Kujifunza Nje.....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha anasimamia haki za wasanii ipasavyo.
Membe alitoa kauli hiyo mkoani Lindi wakati akitangaza nia ya kuwania urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

  • “Nitahakikisha naweka mipango imara katika kusimamia kazi za wasanii wote kunufaika na hakimiliki zao,” alisema.

Pia alisema atahakikisha wasanii wanakwenda kujifunza nje ya nchi masuala ya sanaa ili sekta hiyo ipate mabadiliko ya kimaendeleo kwa wasanii na Serikali kwa ujumla.

  • “Nikichaguliwa kuwa rais, nimejiwekea mikakati mingi kuhakikisha sekta ya sanaa inapiga hatua kutoka hapa tulipo sasa,” alisema Membe.

Katika mkutano huo, waliohudhuria ni baadhi ya wasanii akiwemo mchekeshaji, Adam Melele ‘Swebe’, Hemed Malyaga ‘Mkwere Orijino’ na Kulwa Kikumba ‘Dude’.

Gazeti la Mtanzania


Tanzania Hottest Celebrity Gossip New
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyinyi wasanii mtaahidiwa sana pindi wakaapo katika hivyo viti vyao hata habari na nyinyi hawana wanakuwa busy kuifisadi nchi yao nyinyi wasanii hamna mpango nyinyi inatakiwa mshikame na mjiokoe nyinyi wenyewe mkiwa ngojea hao akina mission impossible na fake promises zao ili wachaguliwe mtajikuta time's runnin'out na mmeishazeeka wewe ulishaona wapi acha TZ tu bali the all Africa waliopo juu baada ya kuchaguliwa wakaja wakawasaidia waliopo chini ili nao wajikwamue kimaisha?

    ReplyDelete

Top Post Ad