Morogoro: Watu watatu wafariki katika mapambano na Polisi, wawili wanasadikiwa kuwa Al Shabaab..Wengine 50 wanasakwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu watatu wamefariki wawili kati yao wanasadikiwa kuwa ni wafuasi wa Al Shabaab katika mapigano baina yao na jeshi la Polisi.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro amesema tukio hilo limetokea eneo la mpakani mwa mkoa wa Morogoro wilaya ya Mvomero na mkoa wa Tanga ambapo watu hao walikuwa wamejificha msituni.

Amesema jeshi hilo linawashikilia watu sita kwa kuhusika na tukio hilo, na kwamba uchunguzi zaidi unafanyika ikiwa ni pamoja na msako mkali katika eneo hilo.

Taarifa kutoka katika hospitali ya mission ya Turian mkoani Morogoro zinasema kuwa maiti tatu zimehifadhiwa hapo ambapo kati ya hizo,maiti mbili zinaonekana kuwa ni za watu wasio raia wa Tanzania huku moja ikiwa ni ya mtu ambaye alijeruhiwa vibaya na badaye kufariki akiwa hospitalini hapo.

MYTAKE: Hivi hawa ni alshabab kweli au kutishana tu au jeshi letu linataka sifa?
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bado hawajakutana nao, acha wajifanyie tu hayo maigizo

    ReplyDelete
  2. MASIKINI TANZANIA TUMERUDI ENZI YA NYERERE, HABARI ZOTE ILIKUWA LAZIMA ZIKACHJWE, ZIPIGWE POLISH NDIYO ZIRUSHWE HEWANI... SASA LEO NA NYIE MNAOGOPA HATA KUPUBLISH COMMENTS ZA WASOMAJI WENU.. mweee

    ReplyDelete

Top Post Ad