Mwanamuziki AY Alikana Penzi la Siti Mtemvu, Azungumzia Beef ya Diamond na Ali Kiba na Mipango ya Ndoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msanii Ambwene Yesaya alimaarufu kama AY amekana kutoka kimapenzi na mrembo aliyevua taji la Miss Tanzania mwaka 2014 Siti Mtemvu, Ay amekana hayo leo alipokuwa katika kipengele cha KIKAANGONI ambacho huwa kinafanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa Kumi alasiri.


Msanii Ambwene Yesaya alimaarufu kama AY amekana kutoka kimapenzi na mrembo aliyevua taji la Miss Tanzania mwaka 2014 Siti Mtemvu, Ay amekana hayo leo alipokuwa katika kipengele cha KIKAANGONI ambacho huwa kinafanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa Kumi alasiri.

Mtaanii kulikuwa na tetesi kuwa msanii huyo alishawahi kufaidi penzi la mlimbwende huyo ambae mwaka jana alilivua taji la Miss Tanzania kutokana na kashfa ya kudanganya umri jambo ambalo lilipelekea kuvuliwa taji hilo, moja ya shabiki wa ukurasa wa facebook wa EATV alitaka kujua kama ni kweli AY alikuwa akifaidi penzi la mlimbwende huyo na ndipo hapo aliposema kuwa suala hilo halina ukweli wowote.

Mbali na kukana kufaidi penzi la Siti Mtemvu mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Zigo amefunguka na kuweka wazi utata juu ya Tuzo mbalimbali zilizotolewa wiki iliyopita na kusema kuwa kama msanii unashindanishwa unapaswa kukubaliaina na ukweli.
"Tunzo naziona zina ubora na upungufu wake,ila kama ukikubali kushindanishwa unatakiwa ukubali matokeo, cha msingi nachoona kura za majaji iwe 70% na watu 30% unajua kwenye tunzo watu hawawezi kukubaliana matokeo asilimia mia, ila nachoona mimi iwe kama tunzo zingine kuwa 70% majaji na 30% watu kuepusha kuchakachua kura na kuchagua kilicho bora maana kuna wakati nguvu ya ushabiki inaharibu ukweli wa matokeo"

Inafahamika wazi kuwa AY alikuwa katika kundi la muziki la EAST COAST TEAM ambalo masikani yake upanga hivyo watu walitaka kujua kama anatofauti yoyote na kiongozi wa kundi hilo King Crazy GK na ndipo hapo AY alipofunguka na kusema kuwa hawana tofauti yoyote ile na sasa wanaishi kama brothers na kusema kuwa wanampango wa kufanya kazi na kundi hilo.
"ECT bado ipo na kina GK na mpango wa kufanya nao kazi upo pale pale ila tunafanya kazi pamoja kama brothers, GK tuko nae sana tu, collabo nitawastukiza mwaka huu ila jua kuwa nitafanya kazi na artist mkubwa sana"
"
Lakini pia AY aliweza kutoa sababu kadhaa ambazo zimemfanya mpaka leo kuendelea kufanya poa kunako soko la muziki wa Tanzania na kusema kuwa moja sababu kubwa ni kutokana na kipaji chake na kujituma pia aelezea umuhimu wa kazi zake za kushirikiana na wasanii wa nje na kusema kuwa kazi hizo ndizo zimefungua njia kwa wasanii mbalimbali sasa kuweza kufanikiwa na hata kwa muziki wetu kupiga hatua zaidi.
"Kukaa muda mrefu kwenye muziki kunatokana na kipaji changu/Utendaji kazi tukija kwenye Collaco na artists wa nje zina matokeo mazuri kwangu na kwa game letu zima la kibongo na napata faraja kwani ndio niliyeanzisha kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwa hapa nyumbani."
Swahiba wa AY ambae ni Mwana FA alinukuliwa siku za karibuni na kusema kuwa haoni faida ya yeye kufanya collabo na wasanii kutoka nje labda itokee wasanii hao wahitaji kufanya nao wao kazi lakini si yeye kuhitaji kufanya nao kazi kutokana na aina ya muziki anaofanya lakini AY leo amesema hata kama swahiba wake hataki kufanya collabo hizo ila atafanya tu kwa lazima.
TEAM DIAMOND VS TEAM KIBA USHABIKI USIO NA FAIDA
Ay amefunguka na kusema kuwa ushabiki unaoendelea sasa hivi kati ya wasanii wakubwa wa bongo fleva kati ya mashabiki wa Diamond na Ali Kiba ni jambo lisilo na faida kwani amefananisha ushabiki huo na kutoa kuwa na faida, adai kuwa ushindani unaopaswa kuwepo ni ule wa kusaidiana kuinuana na siyo ushindani wa kushushana chini hauna faida kabisa katika muziki wetu wa bongo.
"Ushindani wa kusaidiana kuinuana ndio mzuri zaidi kuliko wa kushushana"
Mbali na hilo AY amewataka wasanii mbalimbali ambao wanakuwa wakikimbilia katika siasa na kutaka kuingia bungeni kama sehemu ya kutokea bali wanapaswa kuwa na nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi.
"A.Y wasione ubunge ni sehemu ya kutokea kimaisha, wawe na nia ya dhati kusaidia wananchi"
MAHUSIANO YAKE NA MIPANGO YA NDOA
Mashabiki wamekuwa wakitaka kujua ni kwanini Ay aliachana na Amani na kutaka kujua ni lini haswa mkali huyo atakuja kuoa ndipo0 hapo aliposema kuwa alichana na Amani sababu ya umbali na kusema kuwa suala la ndoa ni mipango ya Mungu.
"Amani bado ni dada na rafiki yangu sana na tuliacha kwa wema kabisa si ubaya,umbali ulitushinda, Kuoa ni Majaaliwa ndugu yangu so akitokea anayestahili nitaoa ,ZIGO ni mwanamke mwenye mvuto ambaye huwezi kumuangallia mara moja"
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NAMPENDA HUYU KIJANA YUPO KAMA ALI KIBA HAWANA MAKUU KABISA NA WANAJIHESHIMU SANA

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha ushabiki wa kijinga ndiyo nyinyi mnaoendekeza team na kwa taariga yako AY hataki mambo ya team

      Delete
  2. ukweli A.Y na Ali Kiba wanafanana kwa mambo mengi. Ni wastaarabu sana . MUNGU AWAJALIE HERI wazidi kusonga mbele.
    Na wengine waigeni hao ili mpate baraka za Mwenyezi Mungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha utem ww sasa Nani ambae unamuon ww kwamba si mstaarabu nongwa hzoo

      Delete
    2. Acha utem ww sasa Nani ambae unamuon ww kwamba si mstaarabu nongwa hzoo

      Delete

Top Post Ad