50 Cent atangaza kufilisika, ni baada ya kupigwa faini ya dola milioni 5 ya kuvujisha sex tape ya ex wa Rick Ross

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rapper 50 Cent amejisalimisha kwa kifungu cha 11 cha sheria ya kufilisika nchini Marekani ili iwe kinga ya kupokonywa mali zake.

Kifungu cha 11 kinayapa muda makampuni kujipanga katika mambo yake kifedha huku yakilinda dhidi ya matakwa ya wanaowadai. Msanii huyo ambaye pia ni mfanyabiashara amewasilisha nyalaka mahakamani zinazoonesha kuwa ana mali na madeni yanayoanzia dola milioni 10 hadi 50, kwa mujibu wa Wall Street Journal.

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mahakama kuamuru alipe dola milioni 5 kutokana na kesi ya kuvujisha mkanda wa ngono wa ex wa adui yake, Rick Ross.

50 Cent alitoa tangazo hilo siku hiyo hiyo aliyotakiwa kupanda kizimbani kwenye mahakama ya Manhattan kuhusiana na adhabu ya faini aliyopewa.

Mwanamke huyo, Lestonia Leviston alitakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha kutokana na kuathiriwa kihisia baada ya 50 kupost online sex tape yake (Leviston) akiwa boyfriend wake wa zamani.

Staa huyo yeye mwenyewe anasikika akiwa kama msimulizi wa video hiyo ya dakika 13 kwa kujipa jina Pimpin’ Curley.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Florida ambaye ana mtoto na Rick Ross alidai mahakamani kuwa video hiyo ilitaka kumfanya ajiue.

Hata hivyo mawakili wa Leviston wamedai kuwa wasilisho la 50 ni njia ya kutaka kukwepa kulipa faini hiyo. Wameomba kuongezwa kwa dola milioni 10 zingine kama ‘punitive damage’ ili kumuadhibu 50 kwa kusambaza mkanda huo.

Hatua hiyo imekuja kama surprise kwakuwa ni miezi miwili tu iliyopita Forbes walidai kuwa rapper huyo ana utajiri wa dola milioni 155.

Jaji wa masuala ya kufilisika anatarajiwa kutoa maamuzi Alhamis hii kama wasilisho la 50 linaweza kuchelewesha kesi hiyo. Hata hivyo rapper huyo anaonekana kutokuwa na stress zozote na kesi hiyo.

Ijumaa iliyopita aliangusha party ya nguvu ya birthday yake huko Las Vegas. Jumapili alitweet, “I can’t remember a year that I had this much fun. Just good energy every were I go.”

Kupitia Instagram, rapper huyo amepost picha hiyo chini na kuandika, “Times are hard out here, LMAO.”

11417491_881388911936507_930719482_n

Vyanzo: Pagesix, BBC News, Billb
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad