Hii Nimeiotoa Kwa Godbless Lema: Kwa nini UKAWA Wamemchukua Lowasa?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KWANINI CHADEMA WAMEMCHUKUA LOWASSA??
(Kama una akili ndogo usisome)
Mnamo mwezi February mwaka huu Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA) waliingia ubia na
kampuni maarufu duniani inayojihusisha na tafiti
za siasa (Political Research) ijulikanayo kama
Greenberg Quinlan Rosner. (
www.gqrr.com/
).
UKAWA walitaka kujua kama wana nafasi ya
kushinda kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kampuni hiyo ilimaliza utafiti wake mwezi May
mwaka huu na haya ndio yalikua majibu;
1. Ikiwa CCM itamsimamisha Lowassa kugombea
Urais, na UKAWA wakamsimamisha Dr.Slaa, CCM
watashinda kwa 58% dhidi ya 42% za UKAWA.
2. Ikiwa CCM itamsimamisha mgombea mwingine
asiye Lowassa kushindana na Dr.Slaa, CCM
itashinda kwa 54% dhidi ya 46% za UKAWA.
3. Ikiwa UKAWA itamsimamisha mgombea
mwingine ambaye si Dr.Slaa na CCM
ikamsimamisha Lowassa, CCM itashinda kwa
68% dhidi ya 32% za UKAWA.
4. Ikiwa UKAWA itamsimamisha mtu mwingine
ambaye sio Dr.Slaa na CCM ikamsimamisha mtu
mwingine ambaye sio Lowassa CCM itashinda
kwa 57% dhidi ya 43% UKAWA.
5. Ikiwa watu wote wa CCM wanaotaka Urais
wakiwekwa Pamoja na wa UKAWA wakawekwa
pamoja kisha wapigiwe kura za Urais kama
wagombea huru, Lowassa ataongoza kwa 14%
kisha Dr.Slaa atafuata kwa 09%, Membe 04% na
wengine chini ya hapo.
6. Ikiwa Lowassa atagombea kupitia UKAWA
atapunguza kura za UKAWA kwa 06% lakini
ataziongeza kwa 24%. Hii ina maana kuwa katika
watu 100 wa CHADEMA watu 6 hawataipigia kura
CHADEMA kwa sababu hawamtaki Lowassa.
Lakini Lowassa ataleta watu wapya 24. Yani
CHADEMA itapoteza kura 6 za wanachama wake
lakini itapata kura mpya 24 mpya.
DATA ANALYSIS
Ukisoma vzr huo utafiti hapo juu utagundua kuwa
Lowassa anaongeza umaarufu wa CCM kwa 18%.
Kwa hiyo kuondoka kwa Lowassa kutaipunguzia
nguvu CCM kwa 18%.
Sasa ikiwa CCM yenye Lowassa ina nguvu 58%
na UKAWA yenye Dr.Slaa ina nguvu 42%, maana
yake ni kwamba kumuondoa Lowassa CCM ni
kupunguza nguvu yao kwa 18% yani (58-18) =
40%.
Na kumleta Lowassa UKAWA ni kupunguza nguvu
ya UKAWA kwa 6% lakini kuongeza kwa 24%. Kwa
hiyo chukua 42 toa 06 kisha jumlisha 24 utapata
60%.
Sasa jumlisha 40% za CCM na 60% za UKAWA
kama haiji 100%??
Kwa hiyo UKAWA yenye Lowassa inashinda
uchaguzi kwa nguvu kubwa zaidi kuliko ambavyo
CCM ingeshinda ikiwa na Lowassa. Na hii ni kwa
sababu ujio wa Lowassa utaivunja CCM vipande
vipande.
Na ili uweze kuishinda CCM lazima uivunje
vipande kwanza. Huwezi kuishinda CCM ikiwa
imesimama imara.
Nchini Kenya KANU ilishindwa kirahisi baada ya
kuvunjwa vipande, Zambia UNIP ilishindwa baada
ya kuvunjwa vipande, na nchi nyingine za Afrika
vivyo hivyo.
Na njia rahisi ya kukivunja chama tawala ni kwa
kuondoa watu wenye ushawishi ktk chama hicho.
Fredrick Chiluba alikua mtu mwenye ushawishi
mkubwa akiwa UNIP lakini alipoondoka kwenda
MMD huo ndio ukawa mwisho wa UNIP maana
alikua na ushawishi na aliondoka na kundi kubwa
la watu.
Nchini Kenya akina Najib Balala, George Saitoti,
Musalia Mudavadi, Raila Odinga, Mwai Kibaki etc
walikua watu wenye ushawishi sana ndani ya
KANU. Lakini walipoondoka kwenda NARC hiyo
ndio ikawa mauti ya KANU.
Hii ni kwa sababu watu hawa walipoondoka,
waliondoka na kundi kubwa la wafuasi. Hivyo
basi hata Lowassa atasaidia kuivunja CCM na
hatimaye kuiwezesha UKAWA kushinda kirahisi.
Ikumbukwe Nyerere aliwahi kusema huwezi
kuishinda CCM imara yenye umoja. Kwa hiyo njia
rahisi ya kuishinda CCM ni kuivunja vunja
vipande. Na tayari kazi hiyo imeanza rasmi.
BAADA YA UTAFITI.
Baada ya ripoti ya utafiti huo wa GNR mnamo
mwezi May, UKAWA walikaa na kutafuta njia ya
kufanya. Walijua wazi CCM ikimpitisha Lowassa
UKAWA itaangushwa hata imsimamishe nani. Na
laiti CCM wangeona ripoti ya utafiti huo
wasingefanya kosa la kumkata Lowassa.
Wangempitisha ili waishinde UKAWA kirahisi.
Kwa hiyo UKAWA walikua wanafuatilia sana
mchakato wa CCM huku wakiomba usiku na
mchana wasimpitishe Lowassa. Na kweli Mungu
akajibu maombi yao.
Lakini UKAWA wakatafakari ikiwa
watamsimamisha Dr.Slaa kushindana na Magufuli
bado UKAWA itashindwa kwa kupata 46% dhidi ya
54% za CCM kama utafiti unavyoonesha.
Kwa hiyo ili kuishinda CCM ni kufanya nini? Ili
kuishinda CCM ni kumshawishi Lowassa ajiunge
na chama kimojawapo kinachounda UKAWA ili
apewe nafasi ya kugombea na kuiwezesha
UKAWA kushinda. Na ndivyo ilivyotokea.
Kwa hiyo kwa mujibu wa utafiti huo UKAWA
itashinda kwa 60% na CCM 40% kwenye uchaguzi
mkuu wa mwaka huu. Sasa nani asiyetaka
ushindi?
Siasa ni hesabu, siasa ni namba, siasa ni sayansi.
Kama hujui hesabu usifanye siasa.
Wavivu wa kufikiri wanaibua hoja uchwara za
ufisadi. Hivi fisadi ndani ya CCM alikua Lowassa
tu? Mbona baada ya kuondoka Lowassa bado
ufisadi umeendelea kushika kasi? Escrow,
Symbion, Meremeta, EPA etc, hivi vyote mbona
vimefanyika bila kuwepo Lowassa?
Acheni akili ndogo, tatizo sio mtu, tatizo ni
mfumo. Tukibadilisha mfumo tumebadilisha kila
kitu. Lowassa hata kama alikua fisadi kitendo cha
kujiunga UKAWA ni rahisi kuacha ufisadi wake
maana amejiondoa kwenye mfumo wa ufisadi.
Lakini kumuweka Magufuli kwny kundi la mafisadi
hata kama yeye sio fisadi lazima alinde mfumo
wa mafisadi uliomuweka.
Ni rahisi kumuokoa mwizi mmoja aliyeingia
kwenye kundi la Watakatifu, kuliko kumuokoa
mtakatifu mmoja aliyeingia kwenye kundi la
makahaba. Mwenye masikio na asikie."
ANGALIZO; Andiko hili nimelicopy na kupaste
kutoka JamiiForums, kwa hiyo unapocomment
hakikisha unazingatia kuwa haya si mawazo
yangu wala msimamo wangu.!
Malisa GJ
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Data Collection/probability + Akili kubwa Unayapata haya mko vizur

    Nanukuu

    Siasa ni mchezo ikibidi badilisha ukkiwa ANGANI
    Chadema imebadili mchezo wakiwa ANGANI

    ReplyDelete
  2. Mmmhhh nimevuta pumzi ndeeefuuu baada ya kusoma yote. Haya bhana tusubirie 60%

    ReplyDelete
  3. Chiluba hakuwaihi kuingia UNIP. Ila alikuwa kiongozi wa wafanyakazi

    ReplyDelete
  4. Kwa hiyo huo mwezi February mpaka May 2015 hao watafiti walishajua kwamba Magufuli atateuliwa na CCM kugombea urais! na pia walishajua kwamba Lowasa ataihama CCM!! Duh hao watafiti kiboko, hebu watutafitie tarehe 5/9/2015 mechi ya taifa stars na Nigeria nani atashinda magoli mangapi, maana hao sio watafiti bali ni wanajim!!

    ReplyDelete
  5. Mnajitahidi kula 'matapishi' yenu, hongereni sana sana. Ni nyinyi chadema ndio mlompa hilo jina la fisadi, na Dr. Slaa akaahidi kumpeleka mahakamani kwani ushahidi anao, leo mnatia 'ulimi puani' BILA HAYA!!!

    ReplyDelete
  6. nonsense peleka mahesabu yako uko

    ReplyDelete
  7. huo ndio ukweli ijapo unawauma akina furani

    ReplyDelete

Top Post Ad