Baba Diamond Akataliwa Kumuona Mjukuu wake Tiffah

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baba mzazi wa mwanamuziki huyo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’.
MSHTUKO! Baada ya hivi karibuni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata mtoto wa kike, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kupitia kwa mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, baba mzazi wa mwanamuziki huyo, Abdul Jumaa ‘Baba D’ amekataliwa kumuona mjukuu wake huyo, Risasi Mchanganyiko lina habari kamili.

ILIKUWAJE?
Kwa mujibu wa baba Diamond, baada ya Tiffah kuzaliwa Agosti 6, mwaka huu, mama mzazi wa nyota huyo, Sanura Kassim a.k.a Sandra alimpigia simu mzazi mwenzake huyo na kumjuza kwamba wamepata mjukuu, jambo ambalo walilifurahia kwa pamoja.

Wakiwa katika mazungumzo hayo kwenye simu, baba Diamond alimuuliza kuhusu sura ya mtoto kama kweli ni wa kwao au siyo kama tetesi zinavyozagaa kwamba siyo wao ambapo alihakikishiwa na mama huyo kuwa Tiffah ni damu yao kwani anafanana na mtoto wao Diamond hasa mdomo.

BABA DIAMOND AFURAHIA
“Nilifurahi sana nilipopigiwa simu na mama Diamond na kuniambia tumepata mjukuu tulipongezana, pia nikamuuliza kuhusu wasiwasi wa kwamba siyo damu yetu kama wengi wanavyodai ambapo alinihakikishia kwamba ni damu yetu,” alisema baba Diamond.

AKATALIWA KUMUONA, APIGWA CHANGA
Baba Diamond alifunguka kuwa, wakiwa wanaendelea na mazungumzo, alimtaka mzazi mwenzake huyo amwelekeze nyumbani ili akamuone mjukuu wake, Tiffah lakini mama D alimpiga ‘changa la macho’ na kumwambia hawapo wameshasafiri kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.

“Niliumizwa sana na maneno hayo kwani yalionesha wazi kwamba, mama D hataki niende kumuona, kwani nyombo vya habari kila siku vinaripoti kwamba Zari na mwanaye wapo hapa Bongo lakini nikaona isiwe shida nikapiga kimya tu,” alisema baba Diamond.
Hata hivyo, baba D alisema kuwa, kutokana na kupigwa changa hilo la macho, hakuweza kwenda kwani hajawahi kufika hata nyumbani kwa Diamond alikohamia huko Madale-Mivumoni jijini Dar na anaona sawa tu kwani hana la kufanya.

UKWELI NI HUU
Kwa mujibu wa mtu wa ndani kwenye familia ya Diamond, ukweli ni kwamba, Zari na mwanaye Tiffah mpaka sasa wako nyumbani kwao na hawajasafiri kwenda Sauz kama alivyoelezwa baba

Diamond mwenyewe hakuweza kupatikana kuzungumzia jambo hilo kwani muda wote simu yake ya mkononi haikupatikana hadi tunakwenda mitamboni.
Source:Globalpublishers
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna kama wazazi Diamond hata maandiko ya Mungu yanatuasa kuwaheshimu wakati wote, hata wewe uliwakosea pengine ukiwa mdogo lakini hawakukutupa ndio maana leo tumekuwa pamoja, nakupenda sana kama shabiki wako lakini kwa hili hebu jaribu kumshirikisha hata mkeo naamini Zari hana makuu atakubali tu babu amuone mjukuu wake

    ReplyDelete
  2. Mzazi ataendelea kuwa mzazi tu. Namshauri Diamond akae na baba yake na wajaribu kutatua matatizo yao. By the way, jina la mtoto "Lattifa" kwa kiarabu maana yake ni "Apple" kwa kiingereza. Beautiful name!

    ReplyDelete
  3. Haya tu husu hii ni ki familia zaidi toeni tofauti zenu kama zipo

    ReplyDelete
  4. mdau huyo Zari ndo hataki ndugu wa Dai, leo unasema amshirikishe kuhusu baba yake? si anajua anataka kumfilisi? zari kaamua kumbambikia mtoto ili amle vizuri, tha baba wa nini tena.

    ReplyDelete
  5. mkewe? alimuoa wapi? kama kuzaa hata paka anazaa.

    ReplyDelete
  6. Makubwa haya dogo nakushauri mambo ya baba an mama ma family usiyaweke hadharani hujui unapunguza mashabiki
    Ingekuwa hadithi za vimwali no problem

    ReplyDelete
  7. huyo dai mambo yake yote anayatoa kwenye habari ya ndani ya famili na ya kikazi na inavyoonekana dai hamshughulikii baba yake hata hali yake ya kimaisha sio nzuri ila wewe mzee hebu tulia kimya itamfunza tu radhi ya baba popote alipo kabla hajafa.

    ReplyDelete

Top Post Ad