HABARI KAMILI Kuhusu Abiria Aliyeuawa Kwa Kupigwa Risasi Kwenye Daladala Jijini Dar na Wengine Kujeruhiwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa wakati watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliposimamisha daladala eneo la Jangwani na kuingia ndani kupora mkoba unaosadikiwa kuwa na fedha.Askari na wasamaria wema wakiwa wamebeba mwili wa abiria aliyepigwa risasi na majambazi akiwa ndani ya daladala eneo la Jangwani, Dar es Salaam jana. Daladala hilo lilikuwa likitoka Kariakoo likielekea Ubungo Mawasiliano. Picha na Edwin Mjwahuzi Watu hao, waliokuwa na pikipiki aina ya boxer, walikuwa wakifuatilia basi hilo linalofanya safari zake kati ya Kariakoo na Mwenge na kulisimamisha eneo la Jangwani saa 7.30 mchana na baadaye kuwaamuru abiria wote wainame kabla ya kuelekea kiti cha nyuma alikokuwa amekaa mtu huyo aliyekuwa amebeba mkoba.
Mmoja wa abiria wa daladala hilo, Rehema Michael alisema wakati basi lao likiwa linaenda taratibu, alimuona mtu aliyekuwa amepakizwa kwenye pikipiki akishuka na kumfuata dereva na kisha kumuelekezea bastola usoni, akimtaka asimamishe gari.

Alisema dereva wao alitaka kukunja kona kuelekea Jangwani, lakini akatii amri na ndipo dereva wa bodaboda alipokwenda nyuma ya daladala na kumtaka mmoja wa abiria aliyekuwa amekaa nyuma ya daladala kutoa begi, huku mwingine akipiga risasi hewani, lakini hakupewa mkoba huo.
“Baada ya kuona yule abiria anakaidi agizo lao, mmoja wa majambazi hao alimpiga risasi ya kichwani na kifuani na kuanguka chini huku yule abiria mwenzake ambaye alipewa begi hilo alishike alilitupa chini na mmoja wa majambazi aliingia ndani ya daladala na kulichukua,” Hashim Ally.

Shuhuda mwingine, Richard Urio alisema wakati uvamizi huo ukitokea abiria walikuwepo ndani ya daladala hiyo akiwemo konda walilazimika kulala chini baada ya kusikia milio ya risasi zilizokuwa zikipigwa hewani, na kwamba baada ya kuchukua lile begi walimpiga risasi abiria mwingine ambaye alikuwa karibu na marehemu baada kuhisi alikuwa akizuia begi lisitolewe.
“Siti ya nyuma walikuwa wamekaa abiria wanne, na wawili kati yao walikuwa wamasai ambao mmoja wapo alikuwa amevaa begi mgongoni ambalo lilichukuliwa na majambazi baada ya kumuua mmoja wa wamasai huku mwingine akijeruhiwa na bastola shavuni,”Urio.

Shuhuda mwingine, Regina Mateso alisema yeye alipanda daladala hiyo eneo la Shakilango na kuwakuta wamasai hao ambao inasemakana walikuwa na fedha nyingi kutokana na maongezi yao.
“Wale wamasai walikuwa wanapigiana mahesabu na wapi kwa kwenda kubadilisha fedha. Yule aliyefariki alikuwa anamwambia mwenzake ukibadilisha hizi dola unapata Sh16 milioni, hivyo inawezekana wale abiria walikuwa na kiasi hicho cha fedha ambacho walikuwa wameweka katika begi la mgongoni,” Mateso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Ilala, Lucas Mkondya alisema tukio hilo limetokea na wanalifanyia kazi .

“Na sisi polisi tumelipata sasa hivi ndio kwanza tunalifanyia kazi likikamilika tutatia taarifa,” Mkonya
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tanzania sasa inatisha...hata mchana watu wanafanya unyama huwo!!!!Sisi tunachotaka ni amani..watu wamejiingiza zaidi ktk siasa na kusahau utu(amani)..majambazi yanatisha..hao viongozi wanafikiria pesa tu na utajir...mtu ukiwa na amani ni bora na mengine yatafuata...chama chenye experience na amani ni Ccm..na hivi mafisadi wote wanahama..na awamu hii wamepata challenge kubwa sana..I'm sure watabadirika sans tu..

    ReplyDelete
  2. Tanzania sasa inatisha...hata mchana watu wanafanya unyama huwo!!!!Sisi tunachotaka ni amani..watu wamejiingiza zaidi ktk siasa na kusahau utu(amani)..majambazi yanatisha..hao viongozi wanafikiria pesa tu na utajir...mtu ukiwa na amani ni bora na mengine yatafuata...chama chenye experience na amani ni Ccm..na hivi mafisadi wote wanahama..na awamu hii wamepata challenge kubwa sana..I'm sure watabadirika sans tu..

    ReplyDelete
  3. NDIO HAYA TUNAYAPIGA VITA SISI UKAWA! TUNATAKA WATU WAISHI KWA AMANI! JE HII NDIO AMANI AMBAYO CCM imeimba kwa miaka 60?

    NINASEMA: PIPOZ'S...PIPOZ PAWA!

    Ninaendelea kusema

    Ni vigumu kuisimamisha nguvu ya UMMA. PIPOZ PAWA! HATA MAGUFULI ALIJISAHAU AKASEMA PIPOZ PAWA katika hotuba YAKE. Nafikiri anakubaliana na sera za ukawa sasa na huenda akaipigia KURA ukawa


    ReplyDelete
  4. tatizo hapo ni AJIRA,unaona sasa hayo ndo wanayo yataka CCM,Wasomi hawana kazi. mpaka ushikwe mkono na mjomba,shangazi,rafiki nk.na ndo mwisho wao mwaka huu..kudaddeki...

    ReplyDelete

Top Post Ad