Tofauti Kati ya Mrema na Lowasa Kwenye Ugombea Uraisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tofauti kati ya Mrema na Lowasa wote wakiwa wametokea CCM na wote wakiwa wagombea uraisi kupitia upinzani walikoingia bila kujua sera za vyama walivyoingia kwa kuwa waliingia chap chap ni kama ifuatavyo

1.Mrema alikuwa akiungwa na makundi ya wasomi waliobobea wakiwemo maprofesa walikuwa tayari kumbeba na kusukuma gari lake kuonyesha upendo wao kwake.Lowasa wasomi wamekaa naye mbali wengi hata kumsikia hawataki kuanzia wasomi wakubwa hadi wadogo.Slaa alikuwa kipenzi cha wasomi

2.Mrema aliungwa na watu wengi wa hali ya chini (walalahoi) ambao walimpenda bure bila gharama yeyote kwa kuwa alijitambulisha kama mlalahoi mwenzao wakawa wanamwunga mkono na kumsindikiza kwa makundi makubwa ya kutisha wakihemka kwa mihemko ya dhati ya kumwunga mkono mgombea wao.Lowasa haungwi mkono na walalahi wengi kwa kuwa kajitanabaisha kama mtu mwenye pesa anayetaka kumkomboa mlalahoi!! Walalahoi wazo la kukubali kuwa tajiri aweza kuwakomboa wengi wanalikataa hivyo Lowasa kumfanya akose waunga mkono kutoka kundi la walalahoi.Walalahoi wengine ambao wako tayari kumfuata ni wale ambao wanaamini kuwa Lowasa ana hela na wanataka pesa zake kwanza ili waandamane naye ana WAFUASI MASLAHI WENGI MNO ambao hawamwungi mkono kwa dhati kama ilivyokuwa kwa mrema.

3.Mrema alipoondoka CCM aliondoka na wafanyabiashara wengi wazawa kibao ambao walikuwa wakinyionyesha wazi na kumchangia hasa kwa ajili ya mbio za uraisi bila woga na kwa mapenzi ya dhati kwa mrema.Lowasa anaoondoka nao CCM ni watu maslahi si watu wenye hela wanaotaka kumsaidia bali wengi ni wale omba omba wavizia pesa za Lowasa wanaosubiri Lowasa atafute pesa awagawie!! Ziwasaidie ubunge,udiwani au katika mishe mishe za maisha yao.Ni watu wenye tamaa ambao wangependa wapenye waingie ndani ya Team lowasa kule kwenye fuko la hela hasa walibomoe.
Makundi ya wengi wanaohama CCM kumshabikia Lowasa ni wachovu kipesa na kimaisha wamepigika.Wanavizia LOWASA

4.Mrema alibebwa na vyombo vya habari bure hakutoa hata thumuni na misafara ya wasindikizaji ilikuwa ni ya bure hakuwapa chochote.Lowasa kuanzia vyombo vya habari visivyokuwa na haya kutwa vinawinda hela yake na wasindikizaji kuanzia bodaboda wanasema HAPENDWI MTU NI POCHI TU alete pochi tuingie barabarani.

5.Mrema alijipambanua kama mpiganaji wa wazi wa ufisadi Lowasa kauli mbio yake ni ya kuondoa CCM ,ufisadi ulimi wake unashindwa hata kutamka

Kwa ujumla Mrema alikuwa na nguvu kubwa kuliko Lowasa ya uungwaji mkono wa dhati.Kwa kuangalia aina ya waunga mkono Lowasa sisiti kusema uwezo wake wa kushinda Uraisi ni mdogo mno.Angekuwa na Sifa za mrema angalau angefurukuta.

Maoni Binafsi Kutoka Kwa YEHODAYA -JF
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. maoni yako yana ukweli, lakini hayana mashiko kwa wakati huu, sasa hivi watu wanataka mabadiliko, na mwamko ni mkubwa!

    ReplyDelete
  2. Weee Laurent kama hujui basi uliza huyo Lwasa kabebwa kama hujui nyinyi vijan ni kuzungumz tu bila kujua lolote, kwanz hapo Ukawa kufany ajiung nao na wamuhakikishee kugombea urais unajua alitoa kiasi gani? hela zenyew unajua anazitoa wapi? mchagua kisha ukione chamtema kuni. Jamaa yuko kweny deal kesho utakua wa kwanz kulia eti inch tumeiuza tazam wenzen wa inch jiran jins wanahangaika ila wewe una aman na uhur sasa usitak kujikogotea mchague badaae utasom number.

    ReplyDelete
  3. Hayo maoni yako binafsi ni KWELI, tena KWELI TUPU, ndio maana hata CCM hawababaiki nae kabisa, hata kama wakiunganisha vyama vyao vyote 20!!

    ReplyDelete
  4. Ulimi wa Lowasa hauthubutu kutamka neno fisadi kwa sababu yeye mwenyewe ni FISADI PAPA kama tulivyo ambiwa na kutangaziwa na hao hao shosti zake chadema, kwahiyo nafsi yake inamsuta kama ilivyo msuta Lipumba akaachia ngazi, sema tu Edo yeye ni 'kauzu'

    ReplyDelete
  5. Duuh! kwa hayo maoni yako TAWIRE baba......

    ReplyDelete
  6. Huna lolote wale woote waliokuwa dodoma wanaimba tunaimani na lowasa nao ni walala hoi eh!? kingunge aliyemtetea naye mlala hoi!? Mwandosya Mlala hoi eh! nchimbi, sofia na hao wanaojitoa kila siku ccm ni walala hoi eh!! Pole sana. UKAWA oyeee

    ReplyDelete
  7. mjinga sna huyo mwandishi ! kawavyulie nguo ccm Malaya weee ! watu wamechoka na uwizi unaleta ujinga.

    ReplyDelete
  8. Ni hiyo hiyo pesa yake ndio ilo'muingiza CDM, huoni wale wasema hovyo akina Tundu Lisu, Mnyika, Slaa wapo kimya kama hawapo, wametahayari lakusema hawana, na hawatathubutu wote kuzungumzia ufisadi........... wanafiki wakubwa.........

    ReplyDelete
  9. mafisadi wote waliokula ela za escrow hujawaona na ujui wanatoka chama kipi?
    maisha huyaoni yanapoelekea? vipi ajira je zinapatikana? so kama huyajui yote hayo jaribu kuyatafutia majawabu then utakua umepata maada nzuuuuuuri yakuongelea na sio hii uliyoileta.

    ReplyDelete
  10. ndivyo ilivyo!

    ReplyDelete
  11. Tangu lini Lowassa akapigania maslahi ya UMMA? kweli TZ inahitaji mabadiliko lakini sio kupitia Lowassa, hatutapata mabadiliko ya kweli. Mvinyo uleule kipya ni chupa tu hapo, mpo?

    ReplyDelete
  12. You nailed it my dear. Ndio maana watu wanakutukana maana hawana nguvu ya hoja ila hoja ya nguvu. Ila unesahau fact moja ambayo watu wanaogopa kuitamka, na mie naisema ni ukabila. Kaskazini kutanufaika sana maana lowassa ni mbinafsi na mafafiki watakumbukwa, ila nyie washabiki wa Lowassa msije m kasema hamkuambiwa.
    Habari ndio hiyo

    ReplyDelete

Top Post Ad