Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi leo imeifuta hukumu iliyomtia hatiani Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na kuamuru arejeshewe Sh1 milioni alizolipa kama faini.
Hukumu hiyo ilitolewa leo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Aishiel Sumari baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Tamari Mndeme kukubali rufaa hiyo.
Mbali na sababu za rufaa zilizowasilishwa mahakamani na wakili wa Mbowe, Peter Kibatala, wakili Mndeme aliiongeza sababu zingine mbili zinaonyesha mapungufu ya hukumu hiyo.
Wakili Mndeme alimweleza Jaji kuwa shitaka lenyewe na maelezo ya shitaka vilikuwa vinatofautiana hivyo kuathiri uhalali wa shitaka na uhalali wa hukumu iliyomtia hatiani Mbowe.
Mbowe alitozwa faini ya Sh1 milioni au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kumshambulia mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa 2010 katika wilaya ya Hai, Nassir Yamin.
Hukumu hiyo iliyolalamikiwa na Mbowe kuwa haikumtendea haki kwani kesi hiyo ilifunguliwa kisiasa, ilitolewa Juni 17 mwaka huu na Hakimu Mkazi wa wilaya ya Hai wakati huo, Denis Mpelembwa.
Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), na mgombea ubunge wa Jimbo la Hai alilipa faini hiyo na kuachiwa huru na Mahakama ya wilaya ya Hai.
After many years
ReplyDeleteOops
Hii tanganya toto tuone mnafanya Kazi
Ili mchakachuwe matokeo
Mmeula na chuya
Mapesa ya USA na Europe hayatoki ngo mkiiba kura CCM
Na uzuri mwaka huu tuna Watu wetu Kila kona
VIVA KAMANDA MBOWE!
ReplyDeletemungu ni mwema. !!!! hongera sana mbowe
ReplyDeleteHaki ya mtu haipotei sema binadamu wanaichelewesha. KAKA MBOWE MBELE KWA MBELE TUPO PAMOJA SANAAAA. Mwenyezi Mungu azidi kuwapigania na kuwapa kifua cha kuyabeba haya maneno ya uchochezi na kuchafuliwa yanayotolewa na maCCM ili MPOTEZO UELEKEO, HAWATAWEZA KWA JINA LA YESU, tuko nyuma yenu na sala zetu kwa Taifa letu tuweze kufika pale tunapopataka.
ReplyDeleteMH
ReplyDeleteMBOWE HUNA AKILI UMESHINDWA FANYA KAZI YA KUUZA MITUMBA BARABARANI
ReplyDeleteMBOWE UMEUZA CHAMA KWA MJINGA MWEZAKO SASA UNAANZA KUTAPA TAPA
ReplyDeleteKAMA MFA MAJI ULITEGEMEA MTASHINDA ILI UIBE VIZURI NA HUYO LOWASA WOTE NI MAFASIDI WAKUBWA