Mke wa Dr Slaa Azua Gumzo Marekani...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wetu WAKATI nyumbani Bongo moto mkubwa umewashwa na mumewe aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, Josephine Mushumbusi amekuwa gumzo Marekani.

Kwa mujibu wa Mbongo aishiye nchini humo akitumia mtandao wake wa Instagram, mara baada ya Josephine kutua nchini humo akiwa na familia, baadhi ya Wabongo waishio humo walipata habari kupitia mitandao ya kijamii, wakaanza kumtafuta.

“Jamani! Nimesikia kwamba, Dk. Slaa na mke wake wapo hapa Marekani. Sasa hamna namba zake? Maana tunataka kuwasiliana na mkewe,” alisema Mbongo huyo.
Baadhi ya wachangiaji walimuuliza kisa cha kumtafutia, alijibu: “Unajua tulisoma kwenye mitandao kuhusu madai ya Mchungaji Gwajima (wa Kanisa la Ufufuo na Uzima) kwamba, yeye (Josephine) amewahi kuanguka mapepo mara kadhaa.

“Lakini sasa hatujawahi kumsikia Josephine mwenyewe akijibu. Maana Gwajima alikuwa akimjibu Dk. Slaa, akaingiza na mambo ya mkewe. Sasa tunataka kujua mke naye anamjibu nini Gwajima?”
Habari zaidi zilidai kuwa, mke huyo amekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali na mada kuu ni mke wa Dk. Slaa kuwa nchini humo, wengine wakitaka kujua kafuata nini.
Wengi wamehoji kama safari yake nchini humo na mumewe ni kwa sababu ya kujificha baada ya Gwajima kumwanika au kuna lingine.Hata hivyo, Mbongo mwingine alitupia kwenye mtandao wake wa Instgram akisema kuwa, ameshakutana na mke wa Dk. Slaa kwenye mgawaha mmoja akila maisha.

“Jamani, mke wa dokta nimekutana naye laivu. Anakula raha tu. Wabongo kule wao bado wanawashiana moto kwenye kampeni,” sehemu ya ujumbe huo ulisomeka hivyo.
Wakati f’lani mwanzoni mwa mwaka huu, mwanamke huyo akiwa na mume wake walikuwa nchini humo ambapo alionekana akiwa kwenye eneo la starehe akiendesha baiskeli.
Hata hivyo, wakati wa kuondoka nchini, Dk. Slaa mwenyewe alisema anakwenda Marekani kwa ajili ya mapumziko na kwamba atatumia kipindi hicho kujiendeleza katika kozi ya lugha na sheria.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waendesha pikpiki wengi wa namna hii Marekani ni Wanaume. Wengi wenye sifa za magenge. Si picha nzuri kwa huyu mama. Labda hajui kutumia nguvu zake kwa ustaababu, au hajui ustaarabu ni nini. Si pesa. Ni elimu iendanayo na matendo yako. Kuna class unapofikia kuwa mke tumaini wa Raisi.si hiii.

    ReplyDelete

Top Post Ad