Sherehe za Mkondo wa Baa Zanogesha Promosheni ya Tusker Fanya Kweli Kiwanjani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mpenzi wa kinywaji cha Tusker na mkazi wa Sinza Rosemary John (Kulia) akifurahi kwa pamoja na Meneja Mipango na matukio-SBL Lulu Mduma (kushoto) baada ya kukabidhiwa zawadi ya fulana kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo ilifunga kambi katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam kusherekea ushindi wa baa zaidi ya sita zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa pamoja ziliibuka washindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

Mkazi wa Mikocheni na mpenzi wa bia ya Tusker Gaspar Makongoro (38) akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (Kusjoto) na balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi (kushoto) wakati promosheni hiyo inayodhaminiwa na bia ya Tusker ilipofunga kambi katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam kusherekea juhudi za wadau katika kufikisha malengo ya maisha promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

Mkazi wa Mwanza na mpenzi wa bia ya Tusker Hillary Minja (katikati) ambaye alikuwepo kwenye promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani akionyesha zawadi yake ya mfuko aliyokabidhiwa na Mtangazaji wa redio Efm na Mshereheshaji wa promosheni hiyo ya Tusker Gadner Habash (kushoto) kwenye hafla ya kuzipongeza baa saba (7) zilizo kwenye mkondo mmoja ambazo kwa pamoja ziliibuka baa za wiki kwenye shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani lililofanyika katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub Anaeshuhudia (kulia) ni balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi.

Mkazi wa Sinza Mohammed Hamisi (27) akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi (kushoto) na mshereheshaji wa promosheni hiyo Gadner Habash (kulia) wakati promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilipofunga kambi katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam kusherekea ushindi wa baa zaidi ya sita zilizo kwenye mkondo mmoja. Baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

Mkazi wa Sinza Bi. Clara Joseph (kulia) akiifurahia zawadi yake ya fulana na mfuko alivyokabidhiwa kwenye shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Meneja mipango na Matukio-SBL Lulu Mduma na (kulia) ni Mtangazaji wa redio Efm na mshereheshaji wa Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash.

Mkazi wa Sinza, Prosper Minja akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Meneja Mipango na Matukio-SBL Lulu Mduma katika shindano la Tusker Fanyakweli Kiwanjani lililofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya sanaa vilivyopo Legho, Sinza jijini Dar es salaam ambapo baa 7 zilizopo kwenye mkondo mmoja ziliibuka baa za wiki kwenye promosheni hiyo ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani baa hizo ni Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

07/09/2014,
Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kwa udhamini wa bia bora Afrika ya Tusker wiki hii imekuja na mvuto wa aina yake baada ya kuzikutanisha na kuzifanyia sherehe baa mbalimbali zilizopo kwenye mkondo/mtaa  mmoja.

Tukio hilo ambalo lilionekana kuwafurahisha wapenzi wa bia ya Tusker lilifanyika wikiendi ya Jumamosi katika mtaa wa Legho, Sinza jijini Dar es salaam ambapo baa zaidi ya 6 zote kutoka Sinza ziliungana kushiriki katika sherehe hizo. Baa hizo ni:- Amigos, Massawe, Dagaa dagaa, Sina Contena, Saa junction, Chua pub na Lucy pub.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sherehe hizo, Meneja Masoko  wa bia ya Tusker Bi. Nandi Mwiyombella alisema mpaka kufikia sasa kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani imepokelewa vyema na wateja wa bia hiyo jijini Dar na hata mikoani ambapo kampeni hiyo pia inaendelea. 

“Promosheni hii ni muendelezo wa Kampeni ya Tusker Fanya Kweli  kama inavyoonekana kwenye mabango na matangazo ya radio pia ni kampeni inayolenga kuleta muamko wa hamasa kwa watanzania waweze kutekeleza malengo yao waliyoyapanga“.

Alisema kuwa katika maisha baadhi ya malengo yanayotarajiwa  ni pamoja na kujenga nyumba, kufunga ndoa, kununua gari  kuanzisha biashara na kadhalika. Mafanikio ni hatua na kila hatua inastahili pongezi na kusherehekea matunda ya mafanikio hayo,bia ya Tusker inatambua juhudi za watanzania ambapo juhudi lazima ziendane na utekelezaji na katika kufanya hivyo basi mtanzania anapiga hatua hivyo kupitia Kampeni hii Bia ya Tusker inampongeza mtanzania kwa kila hatua anayopiga. 

Tunaamini kwamba kupitia Kampeni hii ujumbe huu utawafikia watanzania wote kwa urahisi zaidi.Bia ya Tusker inatoa hamasa na kusema tufanye kweli na Tusker inatambua kila hatua ya maendeleo iliyopigwa.

Bi. Mwiyombella aliongeza kuwa sherehe za Tusker Fanya Kweli Kiwanjani pia zinalenga kujenga uaminifu kwa wateja na kurudisha shukrani kwao huku wakisherekea kwa pamoja na bia waipendayo ya Tusker. Sherehe hizi za mkondo wa baa tofauti ni muendelezo wa kampeni ya Fanya Kweli Kiwanjani; ikiwa na mkusanyiko wenye ari na muamko zaidi na hivyo ni burudani zaidi sambamba na zawadi nyingi zaidi kwa wateja.

Kampeni ya Fanya Kweli Kiwanjani itaendelea mpaka mwisho wa mwezi wa kumi huku sherehe za mkondo wa baa zikitegemewa kuwafikia pia mashabiki wa bia ya Tuskerwaliopo Arusha na Mwanza kabla ya kampeni kufikia tamati.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Top Post Ad