Breaking News: LOWASSA Apinga Matokeo......Aitaka Tume Ya Uchaguzi Kusitisha Mara Moja Utangazaji Wa Matokeo Hayo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndugu waandishi wa habari;
Tumewaita hapa kuwaomba muwaeleze Watanzania wenzetu, jumuiya ya kimataifa na marafiki zetu wengine wa ndani na nje, kwamba hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kote nchini.
 
Hii ni kwa sababu, upo ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba utangazaji wa matokeo hayo umevurugwa kwa makusudi na watendaji ndani ya NEC kwa kusaidiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Katika maeneo mengi ambako matokeo yameshatangazwa mpaka sasa, kilichoripotiwa kuwa matokeo ya uchaguzi wa urais, hakifanani wala kuendana na matakwa halisi ya wananchi.
 
Matokeo mengi yamesheheni udanganyifu, ulaghai na yameandaliwa kwa lengo maalum la kumbeba mgombea wa CCM, John Pombe Magufuli.
 
Katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi, kura zetu zimepunguzwa na kuongezwa kwa mgombea wa CCM; maeneo mengine, kura zilizotangazwa zimetofautiana na idadi halisi ya kura zilizopigwa.
 
Kwa mfano, matokeo yaliyotangazwa na NEC katika majimbo ya Mkoani na Mtambile, kisiwani Pemba, Makunduchi, Kiwengwa, Donge, Tunduru, Tunduma, Same Mashariki, Chambani, Tandahimba, Kilindi na kwingi kwingineko, ni miongoni mwa matokeo yanayothibitisha kuwa hiki kinachotangazwa na NEC, siyo kura za uchaguzi mkuu wa rais. Tunaweza kuiita, “mzimu wa uchaguzi.”
 
Ndugu waandishi wa habari;
Tangu kuanza kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi huu, viongozi wetu wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) – mimi mwenyewe juzi na jana Mhe. Freeman Mbowe, James Mbatia na Profesa Abdallah safari walilieleza kasoro zilizojitokeza katika matokeo ya rais,
  
Hata hivyo, Tume imeendelea kutangaza matokeo hayo, bila kujali kile ambacho tumekieleza na kukilalamikia, kana kwamba tunachokisema ni ujinga, uzushi na uwendawazimu. Hili halikubaliki.
 
Aidha, katika maeneo mengine, likiwamo jimbo la Ubungo, matokeo yaliyoko mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi, yanatofautiana na yale ambayo yamekusanywa kutoka katika vituo vyote vya jimbo hilo.
 
Hali kama hiyo ipo pia katika majimbo yote ambayo wagombea wa CHADEMA na wale wa vyama washirika vya CUF na NCCR – Mageuzi, ama wamekuwa na nguvu kubwa au wameibuka washindi.
 
Upo ushahidi wa wazi ambao, ninyi waandishi mnaweza kwa kutumia uandishi wenu kuuthibitisha kwamba, katika majimbo yote ambako wagombea wa UKAWA wameshinda, TUME imechelea kutangaza matokeo ya urais kwa sababu zinazothibitisha kuwapo kwa mikakati ya hila.
 
Ikumbukwe kwamba matukio yote haya ya NEC kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa yamekuja baada tu ya Jeshi la Polisi kuvamia vituo vyetu vitatu vya kuhesabia kura na kuwakamata wataalam wetu waliokuwa wakipokea matokeo ya kura za rais nchi nzima ambayo hadi uvamizi huo ulipofanyika tulikuwa tukiongoza katika maeneo mbalimbali.
 
Ndugu waandishi wa habari;
Tunaamini kwa dhati kwamba, uvamizi huo ulifanyika mahususi kwa malengo ya kufanikisha uchakachuaji huo ambao sasa tunauona ukiendelea kufanyika kupitia matangazo yanayoendelea kutolewa sasa na NEC.
  
Wakati tukijua kwamba NEC ndiyo mamlaka pekee ya kisheria ya kutangaza matokeo ya urais, tunapenda kuwataarifu Watanzania na jumuiya ya kimataifa kwamba hadi wakati uvamizi huo ulipofanyika kura zetu za urais tulizokuwa tumezikusanya zilikuwa zikionyesha tukiongoza kwa asilimia zaidi ya 60.
 
Kutokana na makosa hayo makubwa na ya makusudi yanayofanywa na watendaji wa NEC, mimi Edward Ngoyai Lowassa, mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Mgombea Mwenza, Juma Duni Haji, tunautangazia umma wa Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, kwamba hatukubaliani na matokeo yanayotangazwa na NEC.
 
Ndugu waandishi wa habari;
Kutokana na makosa hayo makubwa, tunaitaka NEC kusitisha mara moja utangazaji wa matokeo ya urais na kuanza upya kufanya uhakiki wa kile wanacholetewa na wasimamizi wa majimbo ambacho ushahidi unaonyesha kuwapo kwa vitendo vya hila ambavyo vinafanywa na NEC.
 
Ndugu wana habari
Kile kinachofanywa na NEC hapa ndiyo kile kile kinachoendelea kufanywa kule Zanzibar leo na ZEC ambako kunafanyika juhudi kubwa na za makusudi kupora kwa hila na kwa mabavu mwelekeo wa wazi wa ushindi wa Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF anayeungwa mkono na UKAWA, Maalim Seif Sharif Hamad.
 
EDWARD LOWASSA
MGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee kaa kimya na ukubali matokeo ...asiyekubali kushindwa si mshindani...........embu tuachie amani yetu bwana ......watu hatukupendi ndo maana umefeli kila kona isipokuwa kwenu tu ndo wamekuhurumia.......HAPA KAZI TU matumaini peleka Monduli

    ReplyDelete
  2. mzee mamvi anataka uraisi kwamguvu du!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na push up haendi ikulu NGO pumbavu

      Delete
  3. BABU RUDI KWAKO KACHUNGE NGOMBE,

    ReplyDelete
  4. Ahahahahaha acha nicheke kwanza kkkkkkkk jamaa kahama ccm eti wamemuibia kura kaenda chadema sasa kashindwa uraisi na bado kura hawajamaliza hesabu anaanza tena kulalamika hebu huyu mtu alitumwa na nani ili agombee uraisi? sasa hivi atahamia wapi? inchi nyingine kwani amehama ccm eti amekatwa kaenda chadema sasa ni yale yale eheheee atatorok inchi huyu.

    ReplyDelete
  5. UMESHINDWA NENDA ZAKO

    ReplyDelete
  6. HAUNA AIBU NA ULIVYO IBA PESA ZA CCM NA LEO UNAANZA KULALAMIKA KUIBIWA KURA

    KICHAA NINI WEWE

    ReplyDelete
  7. UPINZANI WAMELISHTUKIA GOLI LA MKONO??

    ReplyDelete
  8. LOWASA ULIPO ONA WATU WENGI UKAJUA UTASHINDA WW NI MPUBAVU HUKUJUA KAMA

    KATI YA WATU HAWO KULIKUWA WA VYAMA VINGINE UNA UCHU WA KWENDA IKULU UKAIBE ZAIDI

    ReplyDelete
  9. CCM IMEKULEA TOKA KIJAN A MPAKA UMEKUWA MZEE ATI WATAKA KUIONDOA CHAMA

    CHAMA CHA CCM MADARAKANI WW MJINGA SANA UMESHINDWA FASIDI WW

    ReplyDelete
  10. Una nyoya ya mkasi, kukatwa ni halali yako

    ReplyDelete
  11. Bora ukubali yaishe, tukirudia tena uchaguzi utapata aibu,hata hicho kiduchu ulichopata kitapungua sana.Wewe sio mtendaji,unategemea kutendewa kila kitu,mbaya zaidi unaotegemea wakutendee wana uchu wa madaraka kwa manufaa yao.TUMEONA HATA KWENYE KAMPENI,NA TUMESHTUKA.

    ReplyDelete
  12. NENDA KACHUNGE NG'OMBE KAMA ULIVYO SEMA JE UNA KUKU NA MBUZI ,BATA? PUMBAV

    ReplyDelete

Top Post Ad