Makamba Ampa Makavu Kingunge...Adai Amekosa Hofu ya Mungu Kwa Kusema Uongo Dhidi ya CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yusuph Makamba amemshangaa Kingunge Ngombale-Mwiru kutamka kwamba chama hicho hakijafanya chochote wakati ndiye aliyeshiriki kuandika vitabu kadhaa vya mipango ya chama hicho.

Katika hali ya kumsuta Kingunge aliyetangaza kuachana na CCM hivi karibuni, Makamba alisema mwanasiasa huyo amekosa hofu ya Mungu kwa kusema uongo dhidi ya chama hicho tawala.

Makamba alisema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni za mgombea ubunge Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya CCM, Emmanuel Mwakasaka uliofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mabasi cha Zamani mjini hapa.

“Kutokana na kukosa hofu ya Mungu, kada huyo amekuwa akisema uongo na kufikia hatua ya kutaka mabadiliko bila ya kutafakari kuwa yeye alishiriki kuandika vitabu vinavyoelezea sera za chama hicho,” alisema.

Alitaja vitabu hivyo kuwa ni Mwongozo wa CCM cha mwaka 1971, Mwongozo wa CCM cha mwaka 1981, Mwelekeo wa CCM katika miaka ya 1990 pamoja na Mwelekeo wa CCM katika miaka ya 2000 hadi 2010.

Katibu mkuu huyo mstaafu alisema kutokana na ushiriki wake katika kuandika vitabu hivyo, mtu mwenye busara hawezi kusema kuwa CCM haijafanya kitu katika kuwaletea maendeleo wananchi. Aidha alisema, kama hakuna mabadiliko Kingunge hawezi kukwepa lawama.

Alisema madai ya Kingunge kwamba CCM imekosa pumzi ni kauli inayostahili kupuuzwa kwani aliingia kwenye chama hicho akiwa kijana na sasa ameondoka akiwa mzee, hali inayoashiria kuwa hawezi kuendana na kasi ya mabadiliko ndani ya chama.

Makamba alisema ameshangazwa kwa kitendo cha kada huyo wa zamani wa CCM kumpigia debe mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa wakati walishirikiana kumkataa Lowassa kwenye vikao vya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa madai kuwa ni fisadi, hastahili kuwa kiongozi wa nchi
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mtatoka wote kutetea wizi wenu
    Lowassa Lowassa ndo chaguo letu

    ReplyDelete
  2. katika mababu waliofilisika kisera ni huyu hapa!!! babu makamba empty kabisa!

    ReplyDelete
  3. Mwaka huu
    Hata angeuwepo hai Mwl Nyerere Kama angeipigia kampeni CCM
    Tungemtosa tuu
    It's Lowassa with UKAWA mwaka huu

    ReplyDelete
  4. Mabadiliko
    Kwa maisha ya vigogo wa CCM
    Tumechoka Tumechoka toka toka CCM
    Lowassa Lowassa Na UKAWA
    Viva viva ikulu yetu

    ReplyDelete
  5. ANAROPOKA,,HAJUI ASEMALO

    ReplyDelete
  6. BABU MAKAMBA VIPIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII? SASA KAMA ALIKUWA ANAWAANDIKIA VITABU HARAFU HAMTAKELEZI NA NYIE NDIO WATENDAJI UNALALA MIKA NIN? JIBU HOJA BABA JANUARY, TOKA MWAKA 2005 MPK 2015 UCHUMI UMEKUWA KWA 7.9 TOKA 7% YAAANI NI PIONT 9 TUUUUUUUUUUUUUUUUU NDIO ILIYOOONGEZEKA PAMOJA NA MBWE MBWE ZENU ZOOOOOOOOOOOOOTE HIZO,MPUMZI CCM KWISHINEY MMEBAKIZA MATUSI TU JUKWAANI HAKUNA HOJA WALA SERA SHEMU ONI YUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  7. Mzee kumbuka huu ni mwaka 2015,hv vitabu c vya mwaka huu,Ss kingunge anasema anataka mabadiliko

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mabadiliko ya kutoka ccm kuja chadema na si vinginevyo.

      Delete
    2. http://mtanzania.co.tz/?p=6924

      Delete
  8. Tubuni enyi Walimwengu. Yaliyofichika Hadharani Mungu anayaona.
    Usitumie jina la Mungu vibaya. Kwani Huyu Mungu unayemtaja ungemtumikia Vyema,
    Mgewathamini Watanzani, Mgewaheshimu, na mngewatendea haki Watanzania. Ni Mungu huyuyu huyu anawaambia Watanzania leo kwamba nimesikia sauti zenu.
    Mungu akusamehe wewe na Viongozi wote wa Juu wanchi hii Waliotumia vyeo vya vibaya kuhujumu na kuwasababishia Watanzania mateso makubwa. Naomba mjitafakari, Tubuni, lakini jiweken tayari kulipa matendo yenu. Wengi mmewaua bila sababu au kwa visingizio au kwa woga kwa yale waliyoyajua. Damu zao zisipotee bure. Na wengi wametoweka kwa kuwaweka Kafara, au Sadaka ili mfanikishe ushetani wenu. Mungu ni mkuu, Mungu hanachyo, Mungu atakupa uliombalo lakini utalipa tu. Mungu kakupa Uhuru na maamuzi. Wengi mlitumia vyeo vyenu sawa. Lakini Mungu huyohuyo Atawalipisheni hapa hapa Duniani. Kwa Wale wanaoipigia DEbe CCM wakijua Maovu yote ya CCM na bado wanaichagua CCM. Mungu anasema, Ole wao wanisalitio. Atawatuza Wanyenyekevu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bora yeye asiyeamini mungu
      Wewe mungu unamjuwa
      Acha ushamba mungu ni imani

      Delete
  9. Kingunge hawezi kuwa na hofu ya Mungu, sio ajabu kwani yeye hana dini tangu zamani. yupo yupo tu kama animal

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usimjaji mtu kwa namna hii. Ni Mungu mwenye siro zote za Watu. Wengi washika dini ndio wauaji.

      Delete
  10. Wewe Makamba ndio umwogope Mungu. Mmefanya CCM chama cha familia. Mnafanya mnavyotaka sio ilivyo kikatiba au kisera. Mzee wa matusi tu huna jipya

    ReplyDelete

Top Post Ad