Mwanamke wa Kichina Maarufu Kama ‘Malkia wa Pembe za Ndovu’ Akamatwa Nchini Akisafirisha Pembe zenye Thamani ya £1.62m

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwanamke wa China anayedaiwa kuongoza genge kubwa zaidi la usafirishaji pembe za ndovu barani Afrika amekamatwa nchini.

Akipewa jina la utani “Ivory Queen”, Yang Feng Glan anadaiwa kusafirisha pembe za ndovu 706 kutoka nchini kwenda Mashariki ya mbali.

Glan, 66, anadaiwa kuwa na ukaribu na majangili wa Afrika Mashariki na walanguzi wa China. Anadaiwa pia kuyasaidia kifedha makundi ya majangili zinazoyasaidia kununua silaha na magari na pia kutoa rushwa ili kufanya kazi bila vikwazo.

Mama huyo alifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na anashtakiwa kwa kusafirisha pembe za ndovu zenye thamani ya paundi milioni 1.62 katika kipindi cha mwaka 2000 hadi 2014 ingawa wapelelezi wanaamini amekuwa akifanya kazi hiyo tangu miaka 1980.

Alifikishwa mahakamani akiwa na wanaume wawili raia wa Tanzania ambao wamekuwa wasaidizi wake wakuu. Anaendelea kushikiliwa na polisi.

Kukamatwa kwa mama huyo kumekuja baada ya kuwepo upelelezi wa mwaka mzima na kikosi cha kukabiliana na ujangili.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kimada wa Kinana huyu

    ReplyDelete
  2. Tunataka kujua hao anaowahonga magari na pesa nyingi ni kina nani na wachukuliwe hatua. Na uchunguzi ufanyike kwa kina inawezekana KUNA MKUBWA/WAKUBWA hapo.

    ReplyDelete

Top Post Ad