Sheria ya Mitandao Yamnasa Mwingine...Huyu Aliwatukana TCRA Wenyewe Kupitia Mtandao wa Facebook

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sheria Mpya ya Makosa ya Mtandaoni ya 2015 imeendelea kuonyesha meno yake kufuatia kijana Israel William (20), kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo, akishitakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo dhidi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Akisoma mashitaka dhidi ya mtuhumiwa huyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Renatus Rutatinisibwa, Mwendesha Mashitaka wa serikali Estazia Wilson, amesema kijana huyo alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Septemba 10 na Oktoba 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Estazia amesema mshitakiwa aliandika na kusambaza katika mtandao wa Facebook taarifa zisizo sahihi, kuwa wafanyakazi wa TCRA wamekuwa wakilawitiwa, akijua kuwa taarifa hizo sio sahihi na ni kashfa.

Mshitakiwa huyo amekana mashitaka hayo na upande wa mashitaka umesema uchunguzi wa suala hilo bado haujakamilika.

Mtuhumiwa huyo amepelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Israel anakuwa mhanga wa pili wa sheria hiyo mpya ya makosa ya mtandaoni, kufuatia pia kufikishwa mahakamani kwa mwanafunzi wa Chuo cha DIT Benedict Ngonyani, kwa kusambaza taarifa za uongo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) Jenerali Adolph Mwamunyange amelishwa sumu.

Mwanasheria Mkuu wa TCRA Kalungula, kwa mara nyingine amewaonya vijana dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kuwashauri kufuata kanuni na taratibu za mawasiliano na matumizi ya mitandao hiyo kwa mujibu wa sheria.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu atakayeachwa kwa kutumia vibaya mitandao ya kijamii na kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kamati I kina kinana majizi Na majambazi ya meno yetu ya tembo
    Pole mafunguo CCM hutaweza sorrrrrrrrrrrryyyyyyyyyyyy
    Nenda magerezani kabla uchaguzi
    Utaijuwa CCM

    ReplyDelete
  2. Huko wapo Mramba na yona
    Kisa mkapa
    Bibi ............. Alikuwa anarudi kwa Mramba .......Kwani .......kwa Nani.........
    Jongoo halipandi mti

    ReplyDelete
  3. Huko wapo Mramba na yona
    Kisa mkapa
    Bibi ............. Alikuwa anarudi kwa Mramba .......Kwani .......kwa Nani.........
    Jongoo halipandi mti

    ReplyDelete

Top Post Ad