Baada ya Tanzania Kufungwa 7 Bila na Algeria..Shaffih Dauda Aichana Vibaya TFF, Adai Walikuwa Wanafanya Jitihada za Uongo Kuhadaa Watanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

From The Desk Of Shaffih Dauda:
Moja kati ya matatizo makubwa ya sisi watanzania ni kutokukubali pale ambapo kuna mtu amekuzidi. Mara nyingi huwa tunadharau yule ana nini, mfano mtu ana gali zuri watasema yule kahongwa au kaiba. Hatukubali uhalisia au mafanikio ya mtu ili kujipa changamoto angalau kama sikufikia au kukaribia mafanikio ya aliyekutangulia.

Maana yake ni kwamba zile jitihada za uhongo zilizokua zifanywa na TFF kuwaaminisha watanzania kwamba tunaweza kuifunga Algeria kitu ambacho ni cha uongo kabisa. Ndio maana mimi toka mwanzoni nilikua napinga kwa asilimia zaidi ya 100 kuhusu swala la kuifunga Algeria. Ndio maana tangu mwanzoni nilitoa ahadi kwamba kama Algeria ikitolewa na Tanzania basi nitaenda gerezani, napapenda uraiani ndio maana nilikua na uhakika hilo swala lisingewezekana.

Mpira hauna short cut ni mipango ambayo ipo clear, TFF ilicheza na saikolojia ya watu baada ya wao kushindwa kazi yao ya msingi kusimamia uwekezaji wa soccer. Waliwadharau Algeria, wakaunda kamati ambazo ilikuwa ni njia ya kuwaada na kuwaaminisha watanzania kwamba inawezekana kirahisi kuwafunga Algeria.

Sifurahii matokeo lakini kwa upande mwingine nafurahia. Hii iwe fundisho kwa viongozi ambao wana mentality za kishabiki badala ya kusimamia na kutengeneza misingi thabiti ya kuendeleza soccer letu, wanabaki kuendeleza propaganda za kuwarubuni watanzania.
Shaffih K. Dauda
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata kama lakini lazima tukubali waarabu wanatumia mbinu chafu sana wakiwa kwao na hasahasa wanapokuwa wanacheza kitaifa,kwa klabu ni afadhali kwa kuwa wanaogopa kunakuwa na wachezaji raia wa kigeni.Tushukuru Mungu kama vijana wetu hawakupata madhara na wamerudi salama.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Stars ni wazuri,pamoja na mbinu za waarabu hasa wanapokuwa nyumbani stars siyo ya kufungwa vile kama wangeweza kucheza kwa utulivu na umakini,tofauti ni kubwa stars ya kabla ya Mkwasa na ya sasa,Walichanganyikiwa,walijawa na hasira hasa walipoona refa hawatendei haki.

      Delete
  2. Goli walilopata Algeries katika 37 seconds liliwachanganya sana Taifa stars wakawa hawajui nini wanafanya, walianza kucheza rafu, hamaki, bila kutulizana, over confidence na speed isiyokuwa na faida ila kupoteza pasi zao na mipira yote inayo okolewa ikiishia kwa wachezaji wa Algeries baada ya kufanya kosa mabeki na kipa wao kuruhusu bao la kirahisi walitakiwa watulizane wawe kama hawajafungwa na kucheza kwa makini zaidi kwani walishawajua vipi Algeries wanacheza katika mechi ya mwanzo na badala yake hasira zikawapanda na kupoteza mwelekeo, kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa ni kosa jirekebisheni na fanyeni yaliyo bora katika CECAFA ili mwende mbele, pia system ya mpira Tanzania haiwezi kuwa nzuri mpaka waibadilishe kwa kuzibinafsisha club kwani mfano mzuri wameona kwa Azam klabu ya juzi tu inavyoweza kushindana na klabu kubwa na za zamani mfano wa African Sports, Coastal Union, Young African na Sunderland (Simba), lazima watanzania waende na wakati.

    ReplyDelete
  3. Hakuna shortcut katika mpira, uwekezaji kwa kuanza na vijana wadogo inatakiwa, wala tusilete visingizio kwa goli kipa sababu wote jana tumeona Algeria walituzidi kila idara, pia wako fit, wana nguvu, ubunifu na malengo pia, ila wachezaji wetu hakuna malengo yoyote waliokuwa nao akina Kanavaro wamechoka wanarukaruka tu uwanjani hakuna wanachofanya, narudia yale magoli yalikuwa ni mgumu kwa golikipa

    ReplyDelete
  4. BADO STARS WANAYO NAFASI YA KUFANYA VIZURI KWENYE MICHUANO MINGINE,SI WABAYA KIHIVYO.

    ReplyDelete
  5. Nina huzuni kubwa.lakini nashukuru kwa kusema mapema nilisema humu humu ,kwamba siku zote ushindi wa uwanja wa nyumbani ni asilimia 90 na ushindi wa viwanja vya ugenini ni asilimia 10.chanzo cha aibu hii kubwa ya kitaifa ni kocha wa timu charles mkwasa.aliuharibu ushindi wa hapa nyumbani kwa ufinyu wa mawazo yake na hususani kujiona yeye ni kila kitu anaamuru nani aanze, nani aendelee, nani atoke, na nani aingie.UPENDELEO bila kujali kigezo cha uwezo.7-0 tumepigwa.ni kama deni la taifa,tunadaiwa wote.TATIZO NI KOCHA TUU,MKWASA NI MVURUGAJI.ama katika timu zinazopata matunzo ya hali ya juu,kulelewa na kugharimiwa zaidi Africa ni TAIFA STARS.NDEGE YA WATU 150 BURE, HOTELI SERENA[5 STARS HOTEL] BURE,PELEKWA KAMBI YA MABILLION AFRIKA KUSINI BURE,POSHO NZITO,NENE,KUBWA.MATOKEO=KOROFINDO.FUCK-IN BASTARD.IFUTWE TAIFA STARS,FUTA.TUNAZO KLABU ZENYE UBORA NA HESHIMA KUBWA AFRIKA,YANGA,AZAM,SIMBA WAO WAENDELEE NA MASHINDANO NGAZI YA KIMATAIFA,SIO TAIFA STARS,BOMU KUBWA.

    ReplyDelete
  6. Hivi Shafi Dauda ni muandishi ama? mpaka leo hajui kutofautisha la na ra? gari na gali?

    ReplyDelete
  7. NISIKILIZENI VIZURI.CHANZO CHA MAAFA YA TAIFA STARS NI CCM.USISHANGAE WALA KUGUNA,NI CCM.KWA KUMTUMIA MALINZI[MKUBWA NA MDOGO]CCM IMEKUA IKIPENYEZA`SIASA ZAKE IKIJITAFUTIA UMAARUFU KWA KUJIIMARISHA UWEPO WAKE KWENYE TIMU HII YA WATANZANIA WOTE.TUSIO WANA CCM SIKU ZOTE TUMEKUA TUKIILAANI TFF YA MALINZI KWA ULEGEVU HUU UNAOJENGA CHUKI MIONGONI.JEE MNAUMBUKA ALIFANYA NINI TAIFA JANUARI MAKAMBA BAINA YA MECHI YA STARS NA NIGERIA?KWA JINA LA CCM ALITOA MILLION 15 WATU WAINGIE BURE MRADI USEME CCM OYEE KABLA YA HAPO JARIBIO LA MALINZI KUMUALIKA MGOMBEA MAGUFULI WA CCM LILILAANIWA NA,LIKAKATALIWA VIBAYA.HAMKUCHOKA 2-2 ALIALIKWA MAGUFULI,HAKUTOKEA KAJA SAMIA.MMEKWENDA ALGERIA REKODI=7 NUNGE.HII SIO TIMU YA WATANZANIA,NI YA CCM NA CCM WANA DHAMBI KUBWA YA KUWAIBIA WANANCHI USHINDI WAO WA DHAHIRI TAREHE 25 OCTOBA 2015.ENDELEENI NA CCM,MJIANDAE 8,10,12 HADI 15'WATU WABAYA SANA NYIE.

    ReplyDelete
  8. Yaani kwa mwendo huu wa Taifa Stars wa Tanzania TUMECHOKA, tena hakuna haja kwa Muheshimiwa Rais au serikali kwa jumla kumlimpa kocha na kuihudumia hiyo timu, TFF wamlipe wenyewe kocha na wahudumie timu, hizo pesa za serikali zitumike kukarabati CT-Scan muhimbili.

    ReplyDelete
  9. Unategemea kitatokea nini ulingoni ukiwapambanisha bondia mwenye uzito wa "LIGHT WEIGHT"na bondia mwenye"HEAVY WEIGHT"?Nafikiri jibu lake unalijua

    ReplyDelete
  10. T FF badirisheni jina la timu kuwa TOKA TAIFA STARS KUWA CCM STARS na kwa kuwa ndiyo iliyoshika dola kwa sasa tutawaruhusu tuu ili mwendelezo wa mvua za mabao usiwe tena mzigo wetu na fedheha kuu watanzania wote bali iwe ccm pekee ambayo tayari ina laana ya wizi wa kura na kupindua matokeo ya uchaguzi mkuu wa tanzania uliofanyika jumapili tarehe 25 octoba 2015.

    ReplyDelete
  11. Uwepo wa siasa za ccm taifa stars si wa siri ni dhahiri sana.kitu hiki ni machukizo makubwa sana sana kwa wananchi wa tanzania.tunakuja uwanjani na tunapambana na vimbwanga chungu nzima vya ccm kibao,tele. mabango,vipeperushi,pesa,midomo,ukuda nk. dhamira na shida ya ccm waiteke michezo yote na wanamichezo kama walivyofanya kwa wasanii wakati wa kampeni.baraka hakuna. narudia baraka hakuna,radha hakuna. ni wizi wa mali ya wote uifanye iwe mali ya ccm.pa kuanzia sina pa kuishia sina CCM MAJANGA.

    ReplyDelete

Top Post Ad