Lipumba Aibukia Ofisi za CUF, Ataka JK Aingilie Kati Suala za ZEC

Ibrahim Lipumba 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuiamuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  (ZEC ) kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa uliofanyika Zanzibar ili kuipusha nchi kuingia katika machafuko.

Jumatano iliyopita, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu akisema uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi.

Akizungumza leo kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari tangu alipojiuzulu, Agosti 6, mwaka huu, Lipumba alisema  amelazimika kutoa ushauri baada ya kuona hatari iliyo mbele kama wananchi wa Zanzibar  watanyang’anywa haki yao.

 “Ijumaa ijayo Dk John Magufuli ataapishwa kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania, Kikwete usimwongezee Magufuli matatizo yaliyopo yanamtosha, ” alisema.

Lipumba ambaye alipokelewa na wafuasi zaidi ya 100 kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, alisema Kikwete ahakikishe kabla hajamaliza muda wake wanaiamuru ZEC kuendelea kutangaza matokeo na kuwatangaza washindi wa uchaguzi huo.

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usompenda kaja tena ha ha ha ........habari za hija baba?? Umerudi salama mzee, karibu karibu, kiti chako kipo bado hakijapata mtu, yule usomtaka kishapigwa chini!! Pesa zake wamemlia na kura hawakumpa......

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad