Taarifa ya Serekali Kuhusu Taarifa za Kifo cha Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa Zilizozagaa Mitandaoni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msemaji  Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Assah Mwambene amekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kuwa amefariki Dunia.

Akizungunza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mwambene amesema Rais Mkapa yupo salama na mzima wa afya na hakuna maradhi yoyote yanayomsumbua.

Mwambene amewaasa watumiaji wa mitandao mbalimbali hasa Blogs kuacha kuitumia mitandao hiyo kwa kupotosha umma na kuandika nambo yasiyo na ukweli ili kuepusha mifumuko ya habari za upotishaji.

Si jambo jema na wanaofanya hivyo waache mara moja kabla ya hatua stahiki hazijachukuliwa,” amesema Mwambene.

Amesema kuwa jambo la kumzushia mtu kifo si jambo zuri ambalo amelizungumza kama ‘uchuro’ kwa mtu husika na kumtabiria mabaya.

Mkapa yupo hai na kesho pia atakuwepo katika sherehe za kumuapisha Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli,” amesema Mwmbene na kuongeza.

Serikali italishughulikia hili na tayari imeshaanza kukamata baadhi ya watu mbalimbali ambao wanatoa taarifa za uongo zinazopelekea umma kupotoka.

Amesema kuwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uweredi ili kazi ya uandishi wao iwe ya usawa na kufuata misingi ya uandishi, jambo ambalo wengi hukiuka kutokana kutofuata weredi wa kazi zao.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama kawaida yao CCM
    Kuficha magonjwa hadi vifo kisa shughuli ya kesho
    Kama hajafa kesho awepo kwenye kuapishwa basi

    ReplyDelete
  2. Hilo limewagusa, ila la kunadi fulani MGONJWA MLILIONA ZURI SIYO?!! Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa binadamu mchungu,

    ReplyDelete
  3. Yaani huyu Kipipa na Tezi Dume wakikauka leo, itakuwa ni furaha ya Taifa zima!!.. Huyo mteule wa NEC yupo tu hapo kama kin`gamuzi.

    ReplyDelete

Top Post Ad