Huyu Jerry Muro Ana Matatizo Gani Jamani? Angalia Video Jinsi Alivyoropoka Maneno Yaliyowasikitisha Wengi...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jerry Muro
Jana katika Press Conference pale Jangwani msemaji wa klabu ya yanga jerry muro hakika alitufanya watu wenye akili zetu tena zilizotukuka tuwe na mashaka nae ya kitaaluma na kiuweledi kutokana na kile alichokifanya ambacho nashukuru hakikumfurahisha kila mtu aliyekuwepo pale na hasa hasa wana Yanga wenzake wale wenye uwezo wa kuchambua masuala.

Hivi ni kweli Jerry Muro anajua majukumu hasa ya afisa habari au afisa uhusiano au meneja mahusiano au kurugenzi ya habari, uhusiano na mawasiliano?

Yaliyonifanya hadi nikaamua kuanzisha huu uzi ni kitendo chake ambacho binafsi naweza kukiita ni kama vile ameibaka taaluma na ikiwezekana upesi na haraka sana atuombe radhi wana taaluma na hapa ndipo tutapima uimara wa uongozi wa klabu ya Yanga kama utamwajibisha au na wenyewe utaungana nae Jerry Muro.

Jana pale mkutanoni Jerry Muro wakati akijibu maswali ya wanahabari, ghafla akapotoka katika hoja ya msingi na kuanza kumjibu hovyo msemaji wa klabu ya Simba, Hajji Manara.

Na ili muyaamini haya niyasemayo naomba kama una mwandishi yoyote wa habari ambaye jana alikuwepo pale ukumbini, muulize maneno machafu, ya kejeli, kudhalilisha, ya kishamba na sifa ambayo Muro alikuwa akiyasema pale.

Hapa nitayasema kisha nitawaombeni nanyi humu mnisaidie kuniambia, je msemaji wa timu au taasisi hivi ndivyo anavyotakiwa kutekeleza wajibu wake?

Maneno yenyewe ni kama haya yafuatayo:

" Kwanza huyo Manara ni mpuuzi kabisa na wa hovyo "
" Mtu anakaa uswahilini ataweza kushindana na mimi niishie Mbezi beach? "
" Mimi namiliki gari la kifahari ambalo yeye hana na hatoweza kuwa nalo "
" Isitoshe nina elimu kubwa ya masters degree ambapo yeye hata diploma tu tatizo "
" Nina uwezo sasa hata wa kuoa mwanamke wa kizungu kwa kuwa mimi ni wa kimataifa zaidi "
" Afisa habari gani kutwa anashinidia mihogo pale Magomeni Kagera? "

Hayo hapo juu ndiyo maneno ya msemaji wa Yanga aliyoyasema jana ktk press conference, ila kutokana na pengine hao waandishi kumwogopa au kumpotezea hakuna aliyeyasema au hata kuyazungumzia isipokuwa chombo kimoja tu cha Magic Fm kipindi cha jana usiku. Na nimeamka leo asubuhi hii nikijua kuwa wale waandishi niliowaona jana pale wangeandika hii kitu na kukemea kwa maslahi na maendeleo ya mpira wetu. Cha kushangaza, hakuna print media yoyote iliyoandika hivyo!

Kidume nimeamua kujilipua kama kawaida yangu. Na kwa wale mtakaodhani hizo kauli nilizoziweka hapo juu Jerry Muro hakuzisema, nawaombeni Muangalie Video Hapo chini

Na cha kuchekesha zaidi, hizo kauli chafu zote alizitoa baada tu ya kuulizwa kuwa je, anasemaje kuhusu malalamiko ya timu za Simba na Azam kuwa Yanga inapendelewa na TFF, baada ya TFF kuyafanyia haraka sana marekebisho ya wachezaji wa kigeni, yaliyowaruhusu wachezaji wote wageni waliokuwa na matatizo na taratibu za vibali vya kucheza ligi kuu kuanzia leo, wakati kabla ya mechi ya Simba na Azam klabu ya Simba ilihangaika huko huko TFF ili wachezaji wake Paul Kiongera na Brian Majwega wacheze lakini TFF ikaikatalia Simba tena hadi kwa vitisho?

Nimetema nyongo rasmi na nawaachieni intellectuals na academicians mliopo humu muweze kujadili zaidi, ila naiomba klabu ya Yanga iliangalie suala hili kwa umakini mkubwa mno hasa kwa huyu msemaji wao kwani akiachwa aendelee kuwa na hizi lugha zisizo na staha kuna siku mpira wetu utachafuka na hata kusababisha machafuko makubwa na hadi vifo.

Binafsi nimesikitika mno!​

Angalia Video Hapa


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe mwandishi ni mtu wa hovyo sana,mbona umeshishindwa ku balance story yako kwa kutufanya sisi wasomaji tuamini kuwa Jerry Muro anamatatizo wakati huyo Hajji Manara ndie aliyelianzisha kwa kusema kuwa Huyo Jerry Muro hakuzaliwa kwenye familia inayojua mpira na pia ni mbumbumbu. Kwa hiyo kimsingi huyo Jerry Muro pamoja na mambo mengine inavyoonekana alikuwa anazijibu zile tuhuma zilizoelekezwa kwake na huyo Hajji Manara. Jamani nyie waandishi muwe mna balance story kuliko kuegemea upande mmoja kisa tu ama una chuki binafsi na mtu au hupendelei ule ukweli aliousema.

    ReplyDelete
  2. Oops kukaa mbezi ndo nini
    Kusoma ulaya ndo nini
    Jenga hoja acha ushamba hata mazense na mbagala wapo wasomi vile vile

    ReplyDelete
  3. Jamaa yeye ndio anaonekana shamba ni mropokaji mtu akiwa faida habari wa Timu lazima awe n.a. hekima ya kuongea sio anafanya direct attack

    ReplyDelete
  4. kwani vilabu vya Bongo vina mashindano ya mipasho???

    ReplyDelete
  5. nadhani ule esemi wa limbukeni akipata makalio hulia pwatapwata,, hapo ndo mahali pake mwacheni ajiproud akutegemea kukaa mbezi wala hakuota kumiliki gari ndo anahisi kamaliza kila kitu..

    ReplyDelete
  6. Huo Ni utani tuliozoea kuona hata kina Julio kipindi yupo Simba alikua anatoa maneno Kama muro. Nyie wandishi viazi

    ReplyDelete
  7. WEWE MSENGE NINI AWO WAZARAMO NDIO WALIOKUPOKEA WEWE WAKATI UNAKUJA DAR NA YEBO YEBO FALA WEWE

    ReplyDelete
  8. Muro na Manara wanajuana,waandishi mtabaki mnahangaika na story zao.

    ReplyDelete
  9. Hajui kama club inayomfanya aishi na kuendesha gari ilianzishwa na wazaramo

    ReplyDelete

Top Post Ad