Jinsi Majambazi Walivyotoa Uhai wa Meneja wa Zantel Kwa Kumpiga Risasi.....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Meneja wa operesheni wa kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Zantel, Gabriel Rafael ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.

Tukio hilo limetokea jana saa 4:45 asubuhi eneo la ofisi za kampuni ya Nabaki Afrika, iliyopo Mwenge, mita chache karibu na kampuni ya Coca-Cola.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema haikujulikana mapema meneja huyo alikuwa akitokea wapi na gari lake aina ya Toyota Double Cabin.

Alisema baada ya kupata taarifa za mtu kuuawa kwa kupigwa risasi, polisi walifika eneo la tukio na kubaini kuwa meneja huyo alikuwa amepigwa risasi kwenye kwapa la mkono wa kulia.

Kamanda Wambura alisema ndani ya gari la mfanyakazi huyo walikuta simu, laptop na fedha taslimu Sh1 milioni.

“Mwili wake umepeleka kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala na polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo pamoja na kuwasaka waliofanya mauaji hayo,” alisema Wambura.

Taarifa za mauaji ya meneja huyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana mchana zikieleza kuwa, alikuwa akitokea benki kuchukua fedha.

Katika hatua nyingine, Wambura alitoa rai kwa wakazi wote kutumia njia za kiteknolojia kuchukua na kuhifadhi fedha badala ya kutembea nazo mfukoni.    


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wafanyakazi wenzie idara moja , waliopiga simu the same day, mkewe
    Wote peleka segerea it's simple kupata ukweli
    Haiwezekani Mtu auawe zikutwe 1 million na laptop kwenye gari lake
    Waliopo juu ndo wahusika

    ReplyDelete
  2. poleni ndugu, marafiki na jamaa. Mwenyezi Mungu wapunguzie maumivu makali mliyoyata.

    ReplyDelete
  3. kama ni wezi si wangechukua pesa?

    ReplyDelete
  4. Gabriel umetutoka lakini mimi kama mdogo wako na pia nilifanya kazi na wewe zantel hakika tumepoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya telecom ni mtu mwenye uwezo usiekubali kushindwa mchapakazi mpiganaji na ni rafiki wa kweli bila kujali rika hakika inauma na inasikitisha sanaa mimi umeniachia jambo moja kubwa sana ambalo ni utendaji wa kazi kwa vitendo pia kujiongeza pale unapofanya jambo na hata kama boss basi usisubiri kuletewa jambo pia kuwa mbunifu katika kipind chote nilichokaa na ww tukiwa zantel nimejifunza mambo mengi kutojka kwako rai yangu kwa jeshi la polisi kuahkikisha watu wote waliofanya unyama huu wanakamatwa kama kweli alikuwa na pesa na alitoka benk uchunguzi uanzie bank ni nan alimkabdhi pesa na mawasiliano yafuatiliwe asante sana

    ReplyDelete
  5. Gabriel umetutoka lakini mimi kama mdogo wako na pia nilifanya kazi na wewe zantel hakika tumepoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya telecom ni mtu mwenye uwezo usiekubali kushindwa mchapakazi mpiganaji na ni rafiki wa kweli bila kujali rika hakika inauma na inasikitisha sanaa mimi umeniachia jambo moja kubwa sana ambalo ni utendaji wa kazi kwa vitendo pia kujiongeza pale unapofanya jambo na hata kama boss basi usisubiri kuletewa jambo pia kuwa mbunifu katika kipind chote nilichokaa na ww tukiwa zantel nimejifunza mambo mengi kutojka kwako rai yangu kwa jeshi la polisi kuahkikisha watu wote waliofanya unyama huu wanakamatwa kama kweli alikuwa na pesa na alitoka benk uchunguzi uanzie bank ni nan alimkabdhi pesa na mawasiliano yafuatiliwe asante sana

    ReplyDelete

Top Post Ad