Nampa Kila Anachostahili Mke Wangu Lakini Sina Amani na Ndoa yangu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mke wangu nampenda sana kila anachotaka nampa. Yeye ni mwalimu wa msingi. Uwezo wangu wa kifedha si mkubwa lakini nimejitahidi hadi nimemnunulia walau kigari cha kuendea kazini katika jitihada za kumfanya nae ajisikie vizuri mbele za watu.

Mshahara wake ni chini ya laki 5 lakini huwa namwekea mafuta ya shilingi laki 3 kwa mwezi ili aende kazini. Nampa matunzo yote anayotaka kama mke wa ndoa anavyostahili.

Kinachonisikitisha ni dharau anazonionyesha ndani ya nyumba. Akiamua kunitukana inachukua siku tatu kumaliza matusi. Nyumba haina amani naishi kama mhamiaji haramu. Kuna wakati ananiangalia tu na kunisonya bila kumkosea chochote.

Anadai nikisafiri anaishi kwa amani nikirudi anakereka. Kwa kifupi mimi huwa ni mara chache huwa najibizana nae ninapozidiwa na hasira lakini mara nyingi hukaa kimya.

Nimejaribu kujiuliza ni wapi nakosea sipati jibu. Natunza familia vizuri, unyumba nampa, sina vimada na wala hajawahi kunihisi.

Tatizo ni nini? Nisaidieni wadau niishije na huyu mke? Akiugua anajitahidi kuonyesha jamii kuwa simjali anaamka mapemaa anawahi hospitali ili nionekane simjali.

Akiamua kunitukana anatumia matusi na kashfa nzito dhidi yangu. Bado sijamsimulia mtu yeyote kwa ajili ya kulinda heshima ya familia lakini naona kama nazidiwa.

Naombeni ushauri wenu.

Nafasi za Kazi
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tabia ya wanawake ukiona hivyo teyari kuna mtu anadanganya Mimi ni mwanamke pia hivyo anakutafutia sababu ili umwambie Mimi na wewe basi ajui wanaume wanadanganya ukiwa na mume ukiachika mtu anatoka nduki kama sawa unampenda mkeo ila jifanye kama unamuacha alafu utaona weak nyingi atakuja kukulilia

    ReplyDelete
  2. Jamaani hawa wanawake nafikiri woote tabia zao zinalingana,kila ukimuonyesha unampenda ndio atakufanyia visa hatari, utampa kila aina ya raha na wewe utajinyima lakini hawana shukrani, tena akianza kukusimbulia kwa jambo dogo huwa wanalikariri kila siku.

    ReplyDelete
  3. Hit the road Joe'n'don't come back no more before you do some nasty things to her 'n'regret it after it's too late 'cause she wasn't meant for you Joe'n'don't you worry 'cause the World's gonna hit her very serious

    ReplyDelete
  4. kaa nae chini muulize tatizo n nini...kama kila kitu unatimiza shida ipo wapi....

    ReplyDelete
  5. ulimuoa bila kujua kua mwenzio alikua hakupendi kwa dhati pole sana. chunguza vizuri kabla ya kuoa ndo mana tunaambiwa uchumba usipungue walau mwaka mmoja hadi miwili lkn sk hizi, mmeonana leo, kesho unamwambia nimekupenda, keshokutwa mnafanya ngono, mtondo mnatambulishana kwa wazazi, mtondogoo ndoa tayari..... ni tatizo kubwa sana. tunaendekeza hisia za mwili kuliko roho.

    ReplyDelete
  6. ana jini mahaba alitaki mume mpeleke kwenye maombi

    ReplyDelete
  7. HUYO MWANAMKE HANA SHUKRANI KAKA.WENZAKE WANGEPATA KAMA WEWE MBONA WANGEKULEA USIONDOKE.ANADANGANYWA NA ELIMU YAKE.JARIBU KUM BANIA MATUMIZI.AJUE WEWE PIA UNAWEZA ISHI BILA YEYE.

    ReplyDelete
  8. Dah pole hats Mimi nipo hivyo lkn naombaga msamaha kwa mume wangu baada ya kumchamba sn kln nampempenda kuliko maelezo

    ReplyDelete
  9. pole sana kak lkn me naamin yey c chiz mpaka akafanya hayo yote,cpend kuangalia pande moja inawezekana kuna kosa ulimkoseag na bado hajakusamehe toka moyon, cha msing kaa nae chin kisha mzungumze kam familia naiman mtafika muafaka na kam ulimkosea kuwa mwepes kumuomba msamaha hapo mtapata suluhu ya mchakato mzima.

    ReplyDelete
  10. Huyo ana matatizo ya kiroho hata ukimuacha hata pata mtu wa kukaa nae, kwa tayari ni mkeo hilo ni tatizo lenu, unachotakiwa kufanya tafauta deliverance manual( au kitabu cha maombi yenye upako wa roho mtakatifu) kila jioni kabla ua kulala muwe mnasoma pamoja for one week utaona tofauti sio kwake tu hata kwako wewe mwenyewe

    ReplyDelete

Top Post Ad