Jengo la Ghorofa 16 Mali ya NHC Lilojengwa Chini ya Kiwango Mikononi Mwa Lukuvi..Atoa Siku 18 Jengo Libomolewe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indira Gandhi kabla halijaleta maafa.

Akizungumza jana katika jengo hilo, Lukuvi alisema anashangaa hadi sasa kazi ya kuvunja jengo hilo haijaanza licha ya manispaa kuelekezwa kulivunja.

Uamuzi wa Serikali  kulivunja ulikuja baada kuporomoka kwa jengo katika mtaa huo lililosababisha vifo vya watu 37 na wengine 18 kujeruhiwa mwaka 2013.

“Ni aibu, manispaa mnataka jengo hilo liporomoke na kuua watu tena! Tutachekwa kwa uzembe kama ikitokea tena ajali,” alisema.

Lukuvi alisema kuanzia Februari Mosi uvunjaji wa jengo hilo unatakiwa kuanza vinginevyo wahusika wajiandae kuchukuliwa hatua.

“Nataka nikipita hapa siku yoyote kuanzia mwezi ujao nikute mkandarasi anabomoa jengo hili vinginevyo hatutaelewana,” alisema.

“Hili ni eneo hatarishi hata tuliosimama hapa hatari yoyote inaweza kutukuta lakini Manispaa ya Ilala haioni kwamba hapa kuna tatizo,” alisema.

Waziri alisema uvunjaji wa jengo hilo utakapoanza, wananchi wanaoishi jirani watatakiwa kuhama kwa muda kwa tahadhari.

“Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakianza kuvunja jengo hilo tafadhali waondoeni wakazi wote kwa sababu eneo hili litakuwa hatarishi,” alisema.

Jengo hilo linamilikiwa kwa pamoja kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Ali Raza Investment.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngulumi alisema kilichochelewesha ni makandarasi walioshinda zabuni hiyo kujitoa katika hatua za mwisho wakitoa sababu mbalimbali.

Alisema hivi sasa amepatikana mkandarasi Patty Interplan ambaye yuko katika hatua za mwisho za kupewa kazi hiyo.

“Tutaanza kazi kama ulivyoelekeza,” alisema Mngulumi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, alisema atatoa ushirikiano kwa manispaa hiyo ili kuhakikisha jengo hilo linabomolewa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hasara kubwa hii,sasa sijui kwa taifa au mkandarasi aliyejenga?
    Na hatua gani imechukuliwa dhidi yao,wamesababisha vifo,ulemavu.

    ReplyDelete

Top Post Ad