Nape Toa Mpya..Aitaka Chadema Kumfukuza Edward Lowassa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CCM imemjibu mwanasheria Mkuu wa Chadema ikisema ili chama hicho kikuu cha upinzani kionekane kinapambana na ufisadi kwa vitendo, kinatakiwa kumuunga mkono Rais John Magufuli na kumvua uanachama Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho tawala, Nape Nnauye alisema Chadema iliachana na ajenda ya kupambana na ufisadi baada ya kumpokea Lowassa  Julai mwaka jana baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa CCM kusaka mgombea wake wa urais.

“Sisi hatukumpitisha (Lowassa) awe mgombea wetu wa urais kwa sababu hiyo (ya ufisadi) na ndiyo maana yeye mwenyewe aliamua kuondoka na kwenda Chadema,” alisema Nape.

“Hata katika kampeni za uchaguzi mkuu, Chadema hawakuzungumzia ajenda ya ufisadi, ni kama Lowassa aliifunika tu.”

Alikuwa akimjibu Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu ambaye  juzi alisema ufisadi ni ajenda ya kudumu ya chama hicho kwa kuwa Rais Magufuli hataweza kuufumua wote katika kipindi cha miaka mitano.

Huku akichelea kueleza kiundani sababu za CCM kutomfukuza Lowassa kwa tuhuma za ufisadi mpaka alipoamua kujiondoa na kujiunga na Chadema, alisema kauli ya Lissu inalenga kuwahadaa Watanzania.

“Kauli ya Lissu ni ya kushangaza sana. Sisi tunajua jinsi ambavyo Chadema na washirika wake walivyojitenga na ajenda ya ufisadi. Kama kweli wanaupinga, basi wamuunge mkono Rais Magufuli ambaye kwa sasa anapambana na ufisadi kwa kasi,” alisema mbunge huyo wa Mchinga.

“Wakati mwingine kila jambo hufanyika kwa wakati wake. Suala la kupinga ufisadi CCM lilianza siku nyingi tangu enzi za kujivua gamba. Tumeendelea nalo mpaka watu wakajiondoa wenyewe,” alisema Nape.

Alisema hoja ya kupinga ufisadi ndani ya CCM ilikibeba chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kikapata ushindi mnono, huku Chadema iliyokuwa ikilia na ufisadi ikishindwa.

 “CCM tulieleza sababu za kutompitisha Lowassa kugombea urais na hilo lilikuwa wazi,” alisema.

Katika ufafanuzi wake wa juzi, Lissu alisema ili apambane na ufisadi, Rais Magufuli anapaswa kuacha tabia za CCM na kumtaka mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) amtangaze mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu ambao Chadema wanaamini Maalim Seif Sharif Hamad alishinda.

Pia Lissu alimtaka Rais ataje majina ya waliokwepa kodi ili kama watajitokeza kuwania uongozi, wadhibitiwe kwa kuwa Katiba imezungumza kwa maneno makali dhidi ya vitendo hivyo viovu.

Aidha, aliponda uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo anayetajwa kuhusiska katika sakata la uchotwaji wa Sh3060 bilioni kutoka akaunti ya Tetega Escrow.

Miaka 39 ya CCM

Akizungumzia maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, Nnauye alisema uzinduzi utafanyika Januari 31, visiwani Zanzibar na mgeni rasmi atakuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein.

Alisema kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa Februari 6, mjini Singida na yataongozwa na mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ambaye aliiongoza Serikali ya Awamu ya Nne.

“Viongozi wa kitaifa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu watakaohudhuria maadhimisho haya watapangiwa shughuli za ujenzi wa chama na taifa katika wilaya zote za mkoa wa Singida, siku tatu kabla ya kilele cha maadhimisho,” alisema.

Alisema mikoa yote nchini inapaswa kuandaa shughuli hiyo wiki moja kabla ya maadhimisho, na kwamba lengo ni kufanya shughuli za ujenzi wa chama hicho katika maeneo yao.

“Tutakachokifanya wiki hiyo ni kupokea wanachama wapya, kufanya mikutano ya kuwashukuru wananchi kwa kuiamini CCM na kuichagua iendelee kuongoza, kuhamasisha wananchi kufanya kazi ili kujiletea maendeleo,” alisema.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hueleweki.maraisi wa ccm waliolinda k
    Na kukuza ufisadi hujawasema. Haw ndio waliotupeleka tuliko. Kiwete na nyinyi ndio mnaofuga wauza unga. Boa ndii nyinnyi mlioruhusu. Hibi huna aibu.nawe pia unajificha kwa mutoa mTamshi tu. Huna nia wsla humuungi mkono raisi mGufuli. Utakumbwa tu na ukweli. Wachani Magufuli afanye kazi na mlowassa ndiye aliyewa hemsha. Rudisheni Katiba itakufunga tu.

    ReplyDelete
  2. Kina nape so ndio serikali na ushahidi wa ufisadi wote aliofanya lowasa upo serikakilini kuliko kupiga porojo kwanini wasimkamate lowasa na kumburuza mahakakamani

    ReplyDelete
  3. Jamaa lofa sana hakyamungu dhaa

    ReplyDelete
  4. Kwa nini msiwafukuze kina tibaijuka,chenge,rostam na vibaka wengi waliojaa nyie mafisi.

    ReplyDelete
  5. Badala ya kujibu hoja analeta malumbano kama yuko ngomani!! tena ngoma yenyewe vanga da!!! Halafu naona kama tz inaongozwa na marais wawili vile!! au sasa hivi mtu havai kofia mbili tena bali moja??

    ReplyDelete
  6. Badala ya kujibu hoja analeta malumbano kama yupo ngomani tena ngoma yenyewe vanga da!! Halafu siku hizi kuna rais na mwenyekiti siyo kuvaa kofia mbili tena bali kila mmoja moja!!!

    ReplyDelete
  7. haka ka nepi na unye kameanza tena kuwashwa!

    ReplyDelete
  8. Wewe nape Acha taarabu
    Hapa kazi ya kuhusu nini ya chadema
    Mbona mawaziri mizigo unao kwenye baraza la mawaziri husemi

    ReplyDelete

Top Post Ad