Rais Benjamin Mkapa Naye Ataka Kutumbua Majipu, Amwambia Rais Magufuli Haya Hapa..

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RAIS mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yuko tayari kutoa ushirikiano wa kila aina au kufanya kazi yoyote endapo Rais Dk. John Magufuli atahitaji.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema Mkapa alitoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu na Rais Magufuli.

Ilisema lengo la Mkapa kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na Watanzania kuiongoza nchi, kuunda Serikali na kumtakia heri ya mwaka mpya.

Mkapa amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo,” ilisema taarifa hiyo.

Pia Rais Magufuli alikutana na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba ambaye alisema Watanzania wote wanapaswa kumuunga mkono kiongozi huyo kwa kazi kubwa anazofanya ambazo ni kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali za umma.

Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachia, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais peke yake… yeye awe kiongozi wetu, lakini Watanzania wote tushughulike na matatizo hayo,” ilisema taarifa hiyo ikimkariri Jaji Warioba.

Pamoja na kumtakia heri ya mwaka mpya, Jaji Warioba alimpongeza Rais Magufuli kwa jinsi alivyoanza kazi vizuri, hususani katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi ikiwamo afya na maji.
Kauli ya Mkapa na Jaji Warioba imekuja siku moja tu baada ya juzi Rais mstaafu Jakaya Kikwete kumtembelea Rais Magufuli Ikulu na kufanya naye mazungumzo ambayo hata hivyo yameendelea kuwa ni siri.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wastaafu ndani ya siku mbili kumtembelea Rais Magufuli tangu ameingia Ikulu Novemba 5, mwaka jana.

Udaku Special Blog
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kabla hujatumbua jibu tumbua kwanza tumbo lako lililojaa mali za wananchi. awamu yako iliisha pimbi kaa pembeni acha kutuaribia rais wetu.! hapa kazi tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thank you, you said it well, yeye na mke wake aliuziana mali kibao za serekali, magorofa ya post ilala pale ni ya mama mkapa amboyo sara ni hotel. hugo amend ikulu kusawazisha aliona kiama shake kind kuja. By the way miaka yote hiyo alikuwa wapi mpaka tumble majibu baada JPM kuanza please give us a break. Mwizi namba mona na mkewe.

      Delete
  2. Hahahaha yy mwenyewe tunataka tumtumbue,hiloooo

    ReplyDelete
  3. Fuso wewe ulishindwa ulipokuwa rais
    Jizi kubwa wewe na mkeo ex wife WA Mramba
    Ujuza Tumbo lambo lilijaa laana ya Watanzania

    ReplyDelete
  4. Mtu mzima ovyo
    Kula makombo ya waziri wako
    Fyuuuuuuu
    Mkeo Anna

    ReplyDelete

Top Post Ad