Saed Kubenea kufufua Sakata La Escrow bungeni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (CHADEMA) amesema anatarajia kufufua hoja ya kujadiliwa upya kwa ripoti ya fedha zilizokwapuliwa za Tegeta Escrow zaidi ya Sh bilioni 200.
Akizungumza jana alisema sababu za kutaka mjadala huo kurejeshwa ni kutaka kujua iwapo fedha hizo ni za umma au ni mali ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Sababu nyingine aliyoitaja Kubenea ni kutaka kuchukuliwa hatua kwa wahusika wa sakata hilo, ili iwe fundisho kwa watu wengine.
Iliyokuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika Bunge la 10, iliwasilisha bungeni mapendezo zaidi ya 10 likiwemo azimio namba moja la kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), kumkamata Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pan Africa Power Ltd (PAP) Harbinder Singh Sethi na kumfikisha mahakamani kwa makosa ya utakatishaji wa fedha na ukwepaji kodi.
Kamati inaelekeza Serikali kutumia sheria za nchi, ikiwamo sheria ya Proceeds of Crime Act, kuhakikisha kuwa Singh Sethi anarejesha fedha zote alizochota kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa mujibu wa Taarifa ya CAG iliyothibitishwa na TAKUKURU, fedha hizo pia ziligawiwa kwa watu binafsi.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Zitto Kabwe, alisema kamati yake ilijiridhisha kuwa fedha iliyotumika kulipia manunuzi hayo ni fedha ambayo sehemu yake ni ya umma iliyochotwa bila huruma wala aibu, kutoka Benki Kuu (BoT).
Akaunti hiyo ilifunguliwa na Serikali kwa pamoja kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni ya IPTL.
Fedha hizo zilizua mjadala mkubwa bungeni, ambapo Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliweka msimamo wa Serikali kupitia mkutano wa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, akisema kuwa fedha hizo hazikuwa za umma na hivyo kuzidisha mjadala.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani Kubenea wewe siyo Mtanzania? mbona unaonekana una nongwa utafikiri ulilelewa bila mama? suala hilo tayari lilishaisha na hatua kuchukuliwa na ninavyofahamu taratibu za kibunge wewe pekee yako na UKAWA hamuwezi kuwarejesha watanzania nyuma kwa masuala ya kijinga. Sisi watanzania tuna changamoto nyingi sana na rais na baraza lake linaonekana kutekeleza kwa vitendo na kazi inaonekana acha watanzania wapumzike nyie tafuteni hoja nyingine za kuwaimarisha kisisa badala ya michezo michafu. Rais wako Kubenea kashindwa, subiri hoja yako hiyo ijadiliwe pindi atakapo kuwa rais, acha uwana harakati na umbea wa kwenye magazeti, HAPA NI KAZI TUU, MAJUNGU KWENU. ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete

Top Post Ad