Steve Nyerere Ahenyeshwa Polisi Kwa Utapeli wa Sh Mil 13

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Steve Nyerere
DAR ES SALAAM: Msala! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amedaiwa kuhenyeshwa polisi kutoka na msala wa rafiki yake kuaminiwa fedha za matengenezo ya gari na kuanza ‘kupiga karenda’ matengenezo hayo bila sababu za msingi.

Chanzo makini kimeeleza kuwa, miezi kadhaa iliyopita, Steve alimpeleka rafiki yake aitwaye Mohamed maarufu kwa jina la Mo kwa tajiri wake (jina tunalihifadhi) kisha akamtambulisha kuwa anafanya shuguli za kuuza na kutengeneza magari ndipo Mo alipotumia mwanya huo kuchukua fedha na kumzungusha tajiri huyo.

“Tajiri alivyotambulishwa na Steve kwamba Mo ni rafiki yake, wakabadilishana namba za simu na ndipo siku moja huyo tajiri akampa Mo dili la kutengeneza gari yake iliyokuwa imegongwa kwa shilingi milioni 13, Mo akachukua hela lakini kila akiulizwa lini gari itatoa, hatoi majibu.

“Akawa anapiga chenga, mara niko Sauz mara niko wapi. Sasa huwezi amini tajiri akahisi Steve naye amehusika. Ikabidi ampeleke Polisi Oystebay, akahenyeshwa kwelikweli ili aeleze ukweli anavyomfahamu Mo lakini bahati nzuri akaachiwa baada ya polisi kujidhirisha,” kilisema chanzo hicho.

Alipoulizwa Steve kuhusiana na tukio hilo, hakutaka kufafanua kwa undani zaidi akamuomba mwandishi wetu aachane nalo akidai ‘soo’ hilo wameshalimaliza Mo na huyo tajiri.

“Mi naomba tu uachane nayo hiyo ishu, wameshamalizana wenyewe, lipotezee,” alisema Steve na kukata simu.

Chanzo: GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kanyerere nacho kana kula ugali gn au ndio gym hakana mwili kila siku pamoja kuwa amepora m 13 ataijua namba

    ReplyDelete
  2. Haka kajamaa nimekadharau sana siku hizi!

    ReplyDelete

Top Post Ad