Edward Lowassa: Tutaingia IKULU Kwa Amani Bila Kumwaga Damu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, akizungumza na wazee wa chama hicho, jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam jana walipomtembelea ofisini kwake amewataka wazee hao kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama chao pamoja na ukawa kwa ujuml ili kujiandaana uchaguzi ujao wa 2020.

Lowassa pia ameendelea kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi na kujiepusha na kila jamboambalo wanaona linamwelekeo wa uvunjifu wa amani.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha chama.

Aidha, aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.

"Hali ya chama chetu na UKAWA iko vizuri, uchaguzi tulishinda, sisi tunajua, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda, ila ubabe wao na dhuulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.

Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watazania na ndiyo maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani anasema, "niliwazuia."
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah,kiongozi unaongea nini sasa?
    si ulituambia tukupigie kura tu na ulinzi wa kulinda kura
    utakuwa kwako kwa kuwa unawajua CCM vizuri?

    ReplyDelete
  2. JUMUIYA YA KIMATAIFA WALISEMA UCHAGUZI ULIKUWA WA HAKI.

    ReplyDelete
  3. ZITO NDIO WA KUINGIA IKULU.

    ReplyDelete
  4. Lowasa unazidi kuchanganyikiwa Tu, WW nawe ulikua jipu ulitumbuliwa, sasa naona umejaa tena usaha, JPM haangalii mvi

    ReplyDelete

Top Post Ad