HATIMAYE..Dr Slaa Aibuka..Ajibu Tuhuma za Nyumba yao Kupigwa Mnada Kutokana Kushindwa Kulipa Mkopo wa Sh Million 300

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Katibu Mkuu wa Zamani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa ametoa majibu kuhusu taarifa zinazoandikwa kwenye baadhi ya magazeti nchini pamoja na mitandao kuwa nyumba yake iliyoko Mbezi jijini Dar es Salaam inauzwa baada ya kushindwa kulipa mkopo wa Benki ikidaiwa kuwa mkewe aliuchukua na kumpa mwanaume mwingine.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Mke wa Dk. Slaa, Josephine alichukua mkopo wa shilingi milioni 300 katika moja kati mabenki nchini na kushindwa kuirudisha fedha hiyo.

Dk. Slaa ambaye yuko nchini Canada akijiendeleza kimasomo, amekanusha taarifa hizo na kueleleza kuwa yeye na mkewe Josephine hawajawahi kuchukua mkopo katika benki yoyote nchini.

“Nataka nikuambie na uwajulishe Watanzania kwamba wala si mimi Dk. Slaa wala mke wangu, Josephine kwa wakati wowote ule hatujawahi kuchukua mkopo benki,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu.

“Tangu nitoke Bungeni sijawahi kuchukua hata senti moja benki, achilia mbali propaganda ya shilingi milioni 300.

" Hivyo, ni vizuri waliokupa taarifa wakupe undani ni benki ipi nilikopa au Josephine alikopa na ni shilingi ngapi na kwa nyaraka zipi. 

"Na ni vema ukafuatilia benki husika pia kama walikuwambia ni benki gani,” Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.

Dk. Slaa ambaye alitangaza mwaka jana kustaafu siasa, alisema kuwa anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote walioandika habari hizo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad