Hayawi Hayawi Sasa Yamekuwa....Mrembo Lulu Michael Adaiwa Kulipiwa Mahara...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati akikanusha vikali taarifa mbaya za kuzushiwa kifo mwishoni mwa wiki iliyopita na watu ambao alisema hajui lengo lao, habari ya heri ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani) anaelezwa kuwa kwenye shamrashamra za ndoa baada ya kudaiwa kulipiwa mahari na mfanyabiashara maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa).

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu, hivi karibuni mrembo huyo alilipiwa mahari hayo kwa siri kwa kuwa mwanaume huyo hakutaka mambo hayo yafike kwenye vyombo vya habari.

“Sasa mimi nawapa habari motomoto kuwa Lulu amelipiwa mahari na mwanaume wake wa sasa lakini ishu nzima ilikuwa kwa siri sana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa Lulu (Mbezi-Beach, Dar) na sasa kinachoendelea ni taratibu za harusi lakini jamaa (huyo mwanaume) hataki iwe na mbwembwe.


“Ndiyo maana Lulu sasa hivi ametulia siyo kawaida yake. Hata kwenye viwanja vya bata na shughuli za mastaa haonekani kwa sababu anafanya mazoezi ya kukaa nyumbani kama mke wa mtu.”

Habari hizo zilidai kwamba, Lulu ataolewa ‘soon’ kwani maandalizi yamepamba moto kimyakimya chini ya usimamizi wa mama yake, Lucresia Karugila.

Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilizungumza na Lulu ili kumpongeza kwa kuchumbiwa na kulipiwa mahari kisha kusikia neno lake juu ya ishu hiyo ambapo tofauti na matarajio ya mwanahabari wetu, msanii huyo alikasirishwa na habari hizo huku akiweka wazi kuwa mambo mengine katika maisha yake ni ya binafsi na kwamba siyo kila kitu anaweka wazi kwa watu wengine.

“Hayo ni mambo binafsi, kwenye maisha yangu siyo kila kitu cha kuweka wazi kwa watu,” alisema Lulu kisha akakata simu kwa hasira.

Chanzo:GPL
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wee Amos piga kimya kwani ye ndio wa kwanza kuuuwa na kusamehewa,,,kumbuka U free mason wa kanumba ndio ulio mpelema kuzim lulu kwa nguvu gani za kumsukuma kanumba mpaka afe alikua chambo tu,,,wee ndio una kesi ya kujibu hao watoto unao wa mwaga ukilala na wanawake huoni zambi.

    ReplyDelete

Top Post Ad